KATIKA kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali katika upande wa sekta ya michezo, Mwekezaji wa Simba na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' amesema kuwa klabu ya Simba imeanzisha ushirikiano na klabu ya DC United inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani (MLS).

Akitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Instagram, Dewji amesema ushirikiano huo utakuwa ni wa kudumu kati ya Simba na DC United ambayo ina thamani ya dola milioni 700 (zaidi ya tirioni 1.6 za kitanzania)

Dewji pia ameongeza kuwa ikifika mwaka 2022 klabu ya Simba itasafiri kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi (pre-season) ya msimu wa 2022/23.

Ikiwa huko kwenye Pre-Season Simba itashiriki mashindano ya kimataifa yatakayoandaliwa na timu ya DC United ambayo yatashirikisha timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Marekani (MLS) na timu kutoka Amerika Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...