WAKALA wa Shindano la Miss Kagera  Regina Samwel Zachwa akizungumza machache Mara baada ya kupatikana kwa Mshindi aliebuka  na gari aina ya New Toyota racts
Mrembo aliebuka Mshindi Miss Kagera akiwapungia Mara baada ya kukabidhiwa gari yake aina ya New Toyota racts



  
   Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

WAKALA wa Shindano la walimbwende kutoka Kagera (Miss Kagera) awashukuru wa kazi wa Kagera na viunga vyake kwa kutoa Ushirikiano katika fainali ya Shindano Hilo lililofanyika mwishoni mwa agosti mwaka huu.

Akizungumza na Michuzi Tv Muandaaji wa Shindano Hilo Regina Samwel Zachwa amesema imekua ni Mara yake ya kwanza kuandaa na kupewa kibali cha kuendesha shindano Hilo na muitikio wa wadau na Mashabiki umekua mkubwa na kupelekea jamii kufaidika na kiasi kilichopatikana.

"Nawapongeza wadau na Mashabiki walioweza kufanikisha Shindano la Miss Kagera hakika imekua nafasi nzuri Sana kuona kwa jinsi gani Sekta ya urembo haijaachwa nyuma kwa Mkoa wetu, na mapato tuliyoweza kupata tutarudisha kwenye jamii kama sehemu ya kusaidia jamii yenye uhitaji.

Hata hivyo Zachwa amesema kutoka na kuwepo kwa  Mpango mkakati ambao kila Mrembo anakua na malengo nao kwa ajili ya jamii yake hivyo basi kwa upande wa washindi watatu akiwemo na Mshindi wa Miss Kagera wataweza Kuanza kuitumikia jamii kwa kutoa misaada kwa watoto wenye Matatizo mbalimbali hospitalini pamoja na watu wasiojiweza kupitia mapato yaliyopatikana kupitia viingilio katika Shindano Hilo .

Pia ametaja sababu za Miss Kagera Zuhura Abdul kuibuka Mshindi na kuondoka na gari aina ya New Toyota racts  ni pamoja na nidhamu yake,Mvuto ,akili timamu kichwani huku muonekano ukiwa ndio nafasi pekee iliyombeba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...