Na Mwandishi wetu, DODOMA.

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini hati ya makubaliano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutekeleza Mradi wa kufua umeme wa Megawati 200 kwa kutumia Makaa ya Mawe yanayopatikana Kiwira mkoani Songwe.

Hati hiyo imesainiwa baada ya kukamilika kwa mchakato makubaliano yaliyofanyika Ofisi za TANESCO Makao Makuu Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi na wataalamu kutoka katika Taasisi hizo mbili.

Taarifa iliyotolewa na STAMICO imeeleza kuwa  utekelezaji wa mradi huo unaenda kuyaongezea thamani madini ya makaa ya mawe kwani kwa muda mrefu yamekuwa hayatumiki kimamilifu katika uzalishaji wa umeme kwa ajili ya kulisha kwenye gridi ya Taifa.

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse amesema,kwamba amefurahi kuona Taasisi za Serikali zinashirikiana katika kutekeleza miradi huo.

Pia amesisitiza makubaliano hayo ni mwanzo wa utekelezaji wa mradi huo ambao uaongeza ajira kwa watanzania na kuboresha uchumi wa wazawa wa maeneo hayo.

Ameongeza kwa kusema taasisi hizi mbili zinafanya kazi tofauti lakini zinategemeana katika kuliletea Taifa maendeleo. Hivyo mashirikiano hayo yataiwezesha STAMICO kuongezea thamani katika madini ya makaa ya mawe wakati huohuo TANESCO inapata Malighafi zitakazowawezesha kuzalisha umeme wa kutosha ili kukidhi mahitaji ya nchi na kuwezesha uwepo wa viwanda nchini.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuushukuru uongozi wa TANESCO kwa kushirikiana bega kwa bega tangu STAMICO ilipoanza mchakato wa kuhuisha mradi huu unaolenga kuokoa rasilimali madini zilizopo katika mgodi ili ziweze kuwanufaisha watanzania.

Akiongea kwa upande wa TANESCO Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Tito Mwinuka amesema makubaliano haya ni hatua ya awali inayotoa nafasi kwa kila Taasisi kufanya majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano, ambapo hatua hii itafuatiwa na kufanyika kwa upembuzi yakinifu ili kuweza kubainisha mambo mbalimbali ikiwemo teknolojia na gharama halisi ya utekelezaji wa mradi huu.

Amebainisha majukumu ya kila Taasisi katika makubaliano hayo yatakayodumu kwa muda wa miaka miwili yakuhusisha kufufua mgodi wa chini ya ardhi, kujenga mgodi wa wazi, kujenga mitambo wa kuzalisha MW200 na kujenga njia ya kufarisha ya msongo KV. 400 yenye urefu wa km 100.

Dk.Mwesse ameongeza kuwa faida za mradi huo ; utaongeza kasi ya kusambaza umeme katika maeneo yatakayopitiwa na mradi na kutekeleza lengo la kibiashara la kuuza umeme kwenye nchi Jirani ikiwa ni dhima kuu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini wa Afrika. (SADC).

Pia amesema kuongeza matumizi ya rasilimali nishati kwenye uzalishaji umeme (Power Generation Mix) na kuboresha mifumo ya njia ya kusafirisha umeme.

"STAMICO na TANESCO tumetia Saini Hati ya Makubaliano ya kutekelezaji mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 200 kwa kutumia makaa ya mawe ikiwa ni hatua ya awali utekelezaji wa mradi huo, ambapo STAMICO tutahusika na ujenzi wa mgodi wa wazi wa kuchimba makaa ya mawe, na wenzetu TANESCO watahusika na ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wa MW200 (Power Plant) sambamba na njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Kiwira kwenda Mwakibete na kuunganisha na gridi ya Taifa"ameongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...