Na Heri Shaabani (CHANIKA)
TAASISI ya Fahari Tuamke na Maendeleo imesaidia sekta ya michezo kwa kutoa msaada wa Mipira Club mpya ya Yongwe FC iliyopo Chanika Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala.

Mipira hiyo iliyotolewa na Fahari Tuamke na Maendeleo Dar es Salaam jana katika Bonanza la Michezo lililofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Yongwe ambapo club ya Yongwe FC ilitumia nafasi hiyo kutambulisha club yao ambayo imesajiliwa inajiandaa na ligi ngazi ya Wilaya Ilala .

Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo Mkurugenzi wa TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alisema TAASISI ya Fahari inayomiliki Shule ya watoto Dar Care pia ina timu ya shule hiyo kwa ajili ya kuwaanda vijana katika michezo mbali mbali kwani michezo ni ajira ,michezo mahusiano na michezo ni afya.

Neema alisema FAHARI Tuamke Maendeleo ni Taasisi ya kijamii pia inasaidia makundi mbali mbali ya kijamii ikiwemo sekta ya michezo pia ina Shule ya awali na sasa ipo katika mchakato wa kujenga Shule ya Msingi kuanza darasa la Kwanza .

Alisema wameiwezesha klabu hiyo ili iweze kukuza sekta michezo CHANIKA na Wilaya ya Ilala kwa ujumla.

"Taasisi yetu ya Fahari Tuamke Maendeleo leo imesaidia mipira miwili club hii ya YONGWE FC ili iweze kushiriki mashindano ngazi ya Wilaya ya Ilala mwezi huu "alisema Neema

Alipongeza Serikali ya Mtaa wa Yongwe,Ofisi ya Kata,na Diwani na Ofisi ya Kata kwa kuimalisha Kata ya Chanika na kufanikiwa timu kushiriki mashindano ya Wilaya.

Neema Mchau alimwagiza Kocha wa YONGWE FC kuanzisha timu nyingine ya Watoto wadogi kwa ajili ya kukuza vipaji vyao ili waweze kuandaa wachezaji bora.

wa upande wake Mratibu wa Yongwe FC Kocha wa Klabu hiyo Abdalah Salehe Haule alipongeza klabu Fahari Tuamke Maendeleo kwa msaada huo wa vifaa vya michezo amewataka wadau wengine kuiga mfano huo kuwezesha sekta ya michezo.

Kocha Haule ameomba Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady Kimji kuiwezesha klabu hiyo ili iweze kufikia malengo yake na kuitangaza Chanika na Ilala kwa ujumla.

Aidha Haule aliomba Bonanza lingine lifanyike Baina ya Yongwe na Shule ya Fahari Tuamke Maendeleo.
Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akizindua Bonanza LA Yongwe FC Chanika Wilaya ya Ilala Jana.
kurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akizungumza na Wachezaji wa Yongwe FC iliyopo Chanika Wilaya ya Ilala Dar es Salaam wakati wa kutambulisha club ya Yongwe na uzinduzi wake.
Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akikabidhi mpira kwa Kapteni wa Yongwe FC Chanika Dar es Salaam Jana (Katikati)Kocha wa Yongwe FC Abdalah Salehe Haule PICHA NA HERI SHAABAN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...