VIJANA wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) 'Tamaduni ya Mbinguni, Amani Ulimwenguni na Kurejeshwa kwa Nuru' (HWPL) wameshiriki kupaka rangi katika shule ya msingi ya Kinondoni Julai 31, 2021 jijini Dar es Salaam.

Vijana hao wamepaka rangi katika shule hiyo ya Msingi wakiwa na lengo la kutangaza kazi ya amani hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kupanga rangi katika shule ya msingi kinondoni Mwanachama wa HWPL,Stephen Michael alisema kuwa  vijana hao wanatangaza amani hapa nchini kwa kusaidia jamii na kwa shule ya msingi kinondoni wamesaidia kwa kupaka rangi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Saidi Kibode 
Amewashukuru wana HWLP kwa kuisaidia shule hiyo kwa kupaka rangi katika kuta za madarasa za shule hiyo.

Licha ya hilo Mkuu wa shule aliwaomba wadau wengine wanaoweza kuaidia kama walivyofanya HWPL katika shule hiyo wasaidie kupaka rangi katika madarasa yaliyobakia.

Hata hivyo amewaomba waweze kufanya katika shule nyingine ambazo miundombinu ya madarasa rangi zake zikiwa nimeshachunika.
VIJANA wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) wakindaa rangi kwaajili ya kwenda kupaka katika kuta za shule ya msingi kinondoni jijini Dar es Salaama.

Vijana wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL wakipaka rangi katika shule ya Msingi kinondoni.
Picha ya pamoja ya Vijana wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) mara baada ya kupaka rangi katika shule ya Msingi Kinondoni jijini Daar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...