Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Steve Nyerere ambaye pia ni balozi wa Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es saalam, nakusema kuwa Kuna baadhi ya wanasiasa wamekua wakiwashawishi Watanzania kupitia mitandao ya kijamii wasiende kuchanjwa kwa hiari hali ambayo inasababisha kupoteza uzalendo katika kukabiliana na janga hilo.
" Wapo wanaotumika kisiasa kuhimiza wenzao wasichanje ,kama wewe hauchanji acha watu watumie uhuru wao wa kuchanja au kutokuchanja ,sisi Wazalendo kwanza tumechanja tunahimiza wale wanaowashawishi Watanzania wasichanje kwa hiari yao waacha tabia hiyo" alisema Steve Nyerere.
Ameongeza kwamba " tusitumie mitandao yetu ya kijamii kupotosha Jamii ,mataifa yaliyoendelea yanatumia mitandao ya kijamii kutangaza mambo muhimu kwa taifa lao ikiwemo Sera za Uchumi.
Aidha amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kama Amiri Jeshi Mkuu hivi karibuni alijitokeza kuonyesha uzalendo wa kuchanja, hivyo Watanzania wakiwemo vijana na viongozi mbalimbali wajitokeze kwa hiari kuchanjwa ili wajiweke salama kwa afya zao.
Kwa upande wake msanii wa uigizaji Abdalah Mkumbila maarufu kama Mhogo mchungu aliwashauri Watanzania kuendelea kuchukua hatua za tahadhari kwani Ugonjwa wa Uviko 19 upo na kwamba kundi la watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 ndilo lipo katika hatari zaidi .
" Jitetee mwenyewe kwanza halafu na watu wakutetee,tunaomba Watanzania mjitokeze kwa hiari kupata chanjo na ili taifa liwe na maendeleo lazima wananchi wake wawe wazima" amesema Mhogo Mchungu.
Taasisi ya Wazalendo kwanza imekua mstari wa mbele katika kuhimiza Watanzania hususani vijana kuwa wazalendo katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...