Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa Kuelekea kilele cha Shindano la Urembo Mkoani Kagera, linalofahamika Kama Pilsner Miss Kagera 2021, Kiwanda cha Kuzalisha Maji na kusindika Kahawa cha Tanganyika Instant Cafe (TANICA) kimewalika washiriki wa Shindano hilo kutembelea Kiwanda hicho kilichopo Manispaa ya Bukoba.

Akizungumza na Washiriki hao Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho Rodnes Milton amezitaja shughuli kuu zinazofanywa na Kiwanda hicho ambazo Ni usindikaji wa Kahawa Safi ya Kunywa Aina ya Tanica na Kilimanjaro pamoja na Kuzalisha Maji ya Kunywa ya Tanica Pure Drinking Water, ikiwa ni sambamba na Kahawa ya Vijiweni inayojulikana kwa Jina la Roasted Beans.

Licha ya Warembo kufurahishwa na namna ya uzalishaji wa bidhaa hizo, pia wameonekana kuwa na shauku ya kutaka Kujifunza mengi kupitia maswali waliyouliza kwa Meneja huyo na kupatiwa majibu sahihi.

Aidha Meneja Rodness ameendelea kuwasihi Warembo hao kujiamini, Kujitambua na Kutumia Fursa ya Shindano hilo kufikia malengo yao, na kwamba hata ikitokea mshiriki hakushinda asikate tamaa kwani milango mingine ipo wazi.

Fainali ya kilele Cha Shindano hilo inafanyika Mwezi huu Tarehe 28, 2021 baada ya kumalizika kuwasaka Warembo hao Wilaya zote zinazounda Mkoa Kagera, Shindano lililoanza Mwezi wa Tano mpaka Sasa.












 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...