Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick ndio Wamesaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).
Kupitia mkopo huo, miradi itakayotekelezwa ni katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.
Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.
Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.
Pichani kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick
(kushoto) wakionesha mmoja kati ya mikataba mitano ya mikopo yenye
masharti nafuu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati
ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar, tukio hilo limefanyika jana
jijini Dar es Salaam.
Pichani
kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
(Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick (kushoto),
wakisaini mmoja kati ya mikataba mitano ya mikopo yenye masharti nafuu
yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme,
Tanzania Bara na Zanzibar, tukio hilo limefanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa fedha na Mipango,Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe,Jamal Kassim Ally (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick wakibadilishana mmoja kati ya Mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamanni ya dola za Marekani milioni 292,sawa a shilingi bilioni 674.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyoko katika sekta ya Nishati na kuboresha maisha ya Wananchi wa Zanzibar.Tukio hilo lilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa fedha na Mipango,Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe,Jamal Kassim Ally (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick wakionesha mmoja kati ya Mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamanni ya dola za Marekani milioni 292,sawa a shilingi bilioni 674.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyoko katika sekta ya Nishati na kuboresha maisha ya Wananchi wa Zanzibar.Tukio hilo lilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...