Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Misimu minne nyuma, Soka la Tanzania lilitawaliwa na kushikwa na Matajiri wa mitaa ya Msimbazi, Simba SC, wametwaa mataji ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (Primier League) misimu yote minne mfululizo ya 2017-2018, 2018-2019, 2019-2020 na 2020-2021. Vijana wa Jangwani Young Africans SC walipotea kabisa kwenye misimu hiyo katika Soka la Tanzania.

Simba SC imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Bara  mara nne mfulululizo ni kutokana na Uwekezaji wake katika misingi ya mpira wa miguu si kingine. Maana yake kupata mafanikio makubwa kama baadhi ya timu za Soka barani Afrika kama Al Ahly SC ya Misri na nyingine nyingi zinazosikika na kutamba katika ukanda huu wa Afrika.

Si jambo la kuficha! kwa uwekezaji wa Simba SC katika Soka kupitia kwa Mwekezaji wake na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu hiyo, Mohammed Dewji (MO Dewji). Kupitia uwekezaji huo Simba SC imepata mafanikio makubwa licha ya awali kuwepo kwa kelele nyingi! kwa baadhi ya watu zikibeza na kukebehi uwekezaji wa Mfanyabiashara Mo Dewji wa Shilingi za Kitanzania Bilioni 20.

Tazama, Simba SC imefanya sajili za maana katika kipindi hicho na kutamba katika Soka letu. Sio Soka letu pekee bali hata kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika, Simba SC kwa mara kadhaa imefanya vizuri kwa kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika tena ikidiriki kucheza na timu kubwa, kongwe, maarufu kina Al Ahly, AS Vita Club na wengine kina El Marreikh ya Sudan.

Simba SC imekuwa na Uongozi mzuri hiyo yote ni kutokana na misingi bora ya uwekezaji katika mpira wa miguu. Simba inaongozwa na Mwanadada Afisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez tazama Mwanadada anavyoongoza Jahazi la Simba SC bila kuzama, tazama kwenye miundombinu yake kule Bunju (MO Arena) tazama timu ya Wanawake, Simba Queens leo hii inashiriki Michuano ya ngazi ya vilabu Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake.

Licha ya kuuza Nyota wake, Luis Jose Miquissone na Clatous Chota Chama kwa bei mbaya, Simba wameziba mapengo ya Wachezaji hao kwa kuwaleta Pape Ousmane Sakho, Sadio Kanoute, Duncan Nyoni, Hennock Inonga Baka na Wachezaji wa ndani Yusuph Mhilu, Jimmyson Mwinuke, Israel Patrick Mwenda.

Kwa upande wa Yanga SC, ndio! walipoteana katika misimu minne mfulululizo kama timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu Bara. Lakini kwa uwekezaji wanaoufanya GSM kwa sasa Yanga wameonekana kuwa na ahuheni katika mpira wa Tanzania kuwa sambamba na Watani wao wa Jadi Simba SC. Tazama kwenye usajili wao msimu huu.

Msimu huu wa 2021-2022 ni msimu bab kubwa kwa Vijana wa Young Africans SC wamefanya usajili mzuri mno! kilichobaki ni kazi ya Kocha Mkuu Nassredine Nabi na Benchi lake la Ufundi kutengeneza timu hiyo na kuwa na muunganiko mzuri wa Wachezaji kutokana na wengi ni wapya waliosajiliwa msimu huu wa mashindano.

Yanga SC wameanza vibaya kwenye Tamasha lao la Kilele cha Siku ya Mwananchi, baada ya kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Zanaco FC ya Zambia katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Licha ya kichapo hicho ukitazama timu yao wamefanya sajili nzuri kila idara imekamilila ipasavyo kwa ajili ya mashindano ya ndani na nje.

Yanga SC wana Golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Mali, Djigui Diarra! wana kina Djuma Shaaban, Jesus Moloko, Yannick Bangala, Fiston Mayele wanaounda Kikosi chao na kina Mukoko Tonombe, Yacouba Sogne, Bakari Mwamnyeto na wengine na sasa hivi wapo kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yao! Young Africans wanataka nini???


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...