WANAFUNZI wa bweni katika Shule ya Sekondari Nangomba iliyopo wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara wamesema kwamva wanalazimika kununua maji ambayo yanatokana na mradi wa serikali uliyopo katika vijiji vya Nangomba na Mjimwema wilayani humo.

Wakizungumza shuleni hapo baada ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mkoa huo kutemebelea mradi wa ujenzi wa tenki na bomba ambayo yanatekelezwa na serikali kupitia mradi huo, wanafunzi hao wamedai wanauziwa maji na uongozi wa shule kwa Sh.50 kwa ndoo moja  jambo ambalo linawapa wakati mgumu kutokana na wengi yao kutoka katika familia zisizokuwa na uwezo.

“Tulikuwa tunapata shida ya maji ambapo mda mwingi  tulienda kutafuta maji visimani, kwa sasa tulivyopata maji ya serikali tuna changamoto kwamba maji tunanunua, endapo mtu anakosa fedha inakuwa changamoto kubwa.

"Na kwa sisi wanafunzi wa kike siku zote inatudibidi tuwe wasafi, na kwa hiyo swala la kununua maji bado linatupa ugumu,” amesema Fatma Ismail, mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Nangomba.

mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo Pili Salumu amesema “Mimi binafsi nasikitika sana hili suala la mimi kununua maji shuleni, Serikali imetuletea maji, hata hivyo ilibidi ituangalie wanafunzi, wazazi wetu wengine hawana uwezo wa kutupatia fedha ya kutosha mpaka kununua maji kila siku.”

Amesema yeye hupewa na wazazi wake Sh.2000 tu kwa ajili ya kujikimu akiwa bweni lakini inamlazimu kuitumia kununua maji kila siku na mahitaji mengine kama sabuni ya kufulia na kwamba fedha hiyo huwa haimtoshi.

Said Miraji mwanafunzi wa kidato cha nne ameiomba Serikali itoe huduma ya maji kwa wanafunzi hao bure huku akidai kuwa wao kama wanafunzi sio mda wote wanakuwa na pesa ya kununua maji ikizingatiwa kuwa maji ni moja ya mahitaji muhumu na ya kila mara.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Peter Fransis alikiri kuwa wananfunzi hao wananunua maji ya Serikali kwa madai kubwa shule ina idadi kubwa ya wanafunzi hivyo kuwa ngumu kwa shuel kutoa huduma ya maji kwa watoto.

“Ni sahihi watoto hao wananunua maji kulingana na hali halisi ya shule yetu, hali ni ngumu ‘ku manage’ watoto 300 kwa kuwapa huduma ya maji , sisi kama shule tunachajiwa maji kwa mita,” amesma.

Mwalimu huyo amesema kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanapewa tu maji bure kwa ajili ya usafi  wa vyoo huku akilipia kwa matumizi yao binafsi . Amesema shule hiyo ina wanafunzi 80 ambao ni wabweni.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mariam Chaurembo amethibitisha kuwepo kwa swala la wanafunzi kulipishwa maji huku akisema kwamba serikali ya wilaya inalifanyia swala hilo kazi kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi hao kwa kuwapa huduma ya maji bure.

“Ni kweli nikili kwamba kwenye mradi wetu ule  wa hosteli ambao, watoto  wanauziwa maji, ile hosteli haina chanzo cha maji, serikali imeanza kufanya utafiti tuone kwa namna gani tunaweza kuwapitia maji wale wanafunzi,” amesema.

Akizungumzia mradi huo wa maji, Meneja wa RUWASA wilaya ya Nanyumbu Mhandis Saimon Mchucha, amesema mradi huo wa serikali unatekelezwa katika vijiji vya Nangomba na Mjimwema ambapo hiyo shule ipo katika maeneo ya utekelezaji wa mradi Nangomba.

Katika taarifa yake ya utekelezaji wa mradi aliyotoa kwa kamati ya CCM Mkoa, Mhandisi Mchucha amesema mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 90 una uwezo wa kuzalisha maji lita 6000 kwa saa na unahudumia watu 5500 katika vijiji hivyo.

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo, wameweza kujenga mtandao mrefu wa maji wa kilomita saba na tenki moja la lite 50,000 katika shule ya Nangomba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...