Kwa Kiasi Kikubwa Yaridhishwa na Utekelezaji Wake

Na Mariane Mariane Mgombere, Busega-Simiyu

Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani Busega katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021. Kamati hiyo imefanya ziara ya siku moja Wilayani Busega siku ya tarehe 16 Agosti 2021.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa  na Mjumbe Halmashauri Kuu Taifa Mkoa wa Simiyu Bw. Emmanuel Silanga imeweza kutembelea Miradi ipatayo 7. Bw. Silanga amesema kwa kiasi kikubwa kamati hiyo imeridhishwa na Utekelezaji wa Miradi ambayo imetembelewa.

Aidha, Kamati hiyo imetaka ushirikishwaji wa Utekelezaji wa Miradi mbalimbali kwa Wananchi,  na Viongozi ikiwemo Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji. Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bw. Mayunga George amesema kumekuwa na malalamiko makubwa kwa Wananchi na Viongozi kuhusu kutoshirikishwa Utekelezaji kwa baadhi ya Miradi.

Kwa upande mwingine Bw. Silanga amesema pamoja na kuridhishwa na kazi nzuri ya Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Wilayani Busega, lakini ni muhimu Miradi hiyo kukamilika kwa wakati ili kuondoa changamoto mbalimbali ambazo ni kero kwa Wananchi. Bw. Silanga ameendelea kwa kusema kwamba Wakanadarasi wengi wamekuwa wakichelewesha Miradi mingi hivyo mamlaka husika zisimamie vyema ili Miradi ikamilike kwa wakati uliopangwa.

Pamoja na hayo, wajumbe wa kamati hiyo wameshauri kwamba ni muhimu taarifa za Fedha za Miradi husika ziwe wazi kwa Wananchi. Aidha, kwa upande mwingine wamemuomba Meneja wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Wilaya ya Busega kuwasimamia vyema Wakandarasi wanaoingia nao mikataba ya ujenzi wa Barabara zinazojengwa kuwa na ubora ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.  

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria amesema uongozi wa Wilaya utafanyia kazi maeneo yote yanayoonekana kuwa na changamoto na kuiahidi Kamati hiyo kwamba mapungufu yote yatafanyiwa kazi. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Busega Bi. Veronica Sayore amesema kwamba ana imani kubwa ya kuendelea kutekeleza Miradi ya Maendeleo na kwamba maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo ili kufikia malengo ya Serikali katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni mradi wa ujenzi wa Zahanati ya imalamate ambayo mpaka sasa umegharimu zaidi ya Tshs Milioni 48, ujenzi kilomita 22 barabara ya Busami-Mwanangi na Bombabija-Kajila Katekista kwa thamani ya zaidi  Tshs Milioni 100, mradi wa ujenzi wa wodi 3 Hospitali ya Wilaya; Wodi ya Wanaume, Wanawake na Watoto kwa thamani ya Tshs Milioni 500, mradi wa miundombinu ya Madarasa na Maabara katika Shule mpya ya Sekondari Venance Mabeyo ambapo mpaka sasa thamani iliyotumika ni zaidi ya Tshs Milioni 92, ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Mwabasabi kwa thamani zaidi ya ya Tshs Milioni  72.8, na mradi wa ujenzi wa tanki la maji Kata ya Mkula kwa thamani ya Tshs Bilioni 2.1.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...