Na Abe Paul,  Jeshi la Polisi Arusha


WANAFUNZI watatu katika Shule ya Msingi Ngoile wanaoishi Kijiji cha Ngoile wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamefariki dunia baada ya kuliwa na Simba.

Akizungumza tukio hilo leo Agosti 5,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema watoto hao wameuwa Agosti 3 mwaka huu na amewataja wanafunzi hao ni Olobiko Metui(10),Ndaskoi Sangu(9) na Sanka Saning'o( 10) ambao wote ni wanafunzi wa darasa la tatu."Watoto hao kabla ya kuuawa alishambuliwa na Simba."

Pia mtoto mwingine aitwaye Kiambwa Lektonyi(11)alijeruhiwa na kundi hilo la  simba ambao jumla yao ni watoto wanne wote wanafunzi wa shule ya msingi Ngoile.

Kamanda Masejo amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni baada ya wanafunzi hao  kutoka shule ambapo walifika majumbani mwao na walikwenda kutafuta mifugo yao iliyokuwa imepotea porini kitendo kilichopelekea kushambuliwa na wanyama hao wakali aina simba.

Ameleza kuwa majeruhi  amelazwa katika Zahanati ya Kata ya OLBALBAL kwa matibabu zaidi pia Miili ya marehemu wote imefanyiwa uchunguzi wakidaktari na  ndugu warehemu wamekabidhiwa miili hiyo.

Ametoa mwito kwa jamii za kifugaji kuchukua tahadhari kwa watoto wadogo pindi wanapowapa majukumu ya uangalizi (kuchunga) mifugo hususani katika vijiji vinavyopakana na hifadhi ili kuepusha madhara makubwa ambayo yaweza kutokea katika majukumu yao ya uangalizi wa mifugo pamoja na familia zao.

Pia niendele kuwasihi wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha vitendo vya kiahalifu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...