AMADA Tindwa na Mshamu Tindwa  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha, wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha zaidi ya kilo 50 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Upendo Mono amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Mushi kuwa mshtakiwa Amada anadaiwa kutenda kosa Julai 21,2021 huko Kikobo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.

Inadaiwa siku hiyo mshtakiwa alikutwa akisafirisha kilo 30.4 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Aidha,  inadaiwa siku hiyo katika kijiji cha Tawi wilayani humo mkoa wa Pwani, mshtakiwa Mshamu alikutwa akisafirisha kilo 26.69 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Wakati huo huo, Ally Momboka amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joyce Khoi akikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilo 31.78 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Momboka anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 21,2021 katika kijiji cha Tawi, Wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.

Hata hivyo, washtakiwa wote watatu wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa sababu kiasi cha dawa za wanachodaiwa kusafirisha ni kikubwa na hakina dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 19,2021 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...