Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jeshi la polisi mkoani njombe linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa miundombinu ya vipuri kutoka kwenye kiwanda cha serikali cha dawa na vifaa tiba kinachoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya kupatikana kwa vipuri aina ya mota nne kwenye wilaya ya kipolisi mjini Makambako,kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issa amesema tayari jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwemo walinzi wa kiwanda hicho kilichopo katika kijiji cha idofi mjini makambako.
“Kiwanda
hiki hakijaanza kufanya kazi lakini kuna baadhi ya wtumishi na wananchi
wanaokaa maeneo ya karibu na kiwanda wameweza kushirikiana na kuiba baadhi ya
vipuri katika hawa watu tisa kuna walinzi wako mle,waliozinunua,
Kutokana na jitihada za jeshi la polisi kufanikisha kupatikana kwa vipuri hivyo vilivyoibwa, kamanda issa ametoa wito kwa baadhi ya wananchi na wataalam mkoani njombe waliopewa dhamana ya kujenga na kusimamia miradi ya maendeleo kuwa waadilifu na wazalendo.
“Yeyote anayepangiwa kazi ya ulinzi tanguliza uzalendo na uaminifu katika kazi ya ulinzi na sio vinginevyo”aliongeza kamanda Issa
Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa na vifaa tiba, mhandisi Shiwa Mushi amezungumzia namna walivyobaini wizi wa vipuri hivyo.
“Kwa hiyo kupatikana kwa Motor hizi kuna kazi zitaweza kukamilika vizuri,tunaomba wananchi na wafanyakazi tuweze kushirikiana ili kukamilisha ujenzi huu na ukikamilika utaweza kuajili watu 100 hii ni kazi ya nchi”alisema mhandisi Shiwa Mushi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...