Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Kazi, Ajira,bunge ,Uratibu, Vijana na wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama amezionya taasisi za fedha zilizoanzishwa kwa lengo la kutapeli wastaafu kwa mikopo ya riba kubwa isiyo na tija.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua na kufunga Semina kwa Wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Uhifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF) Jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu "Elimu ya uwekezaji kwa Maisha endelevu baada ya Kustaafu".

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mhagama amesema kumekuwa na changamoto ambazo wastaafu wamekuwa wakikumbana nazo baada ya kustaafu na wakati mwingine kabla hata ya kustaafu ikiwa nii pamoja na kutapeliwa fedha zao.

Amesema wakati mwingine inawezekana watumishi ambao wanashughulikia maisha yajayo ya mstaafu ni watu ambao wanaungana na matapeli kuwatapeli wastaafu kwa maana matepeli wengine huja na taarifa sahihi za mstaafu.

"Niwaombe Wastaafu Watarajiwa kuweni na utaratibu maalumu wa kutoa taarifa ukiona wanaohisiwa ni matapeli ili tuweze kuwakamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.Kupitia hivyo tutaweza kuepukana na utapeli unaotokea mar kwa mara kwa wastaafu wetu". Amesema Waziri Mhagama.

Amesema kupitia mafunzo hayo ni wakati mwafaka kumsaidia kuwaza kujipanga na kufanya maamuzi kuliko kumuacha akafanya maamuzi baada yya kustaafu.

"Ipo miradi mingine inatakiwa ikue kwa utaratibu kama anavyokua mtoto kwahiyo wastaafu wetu wanauwezo wa kusaidia kuitambua miradi ambayo inachukua muda kukua lakini baada ya miaka mitano mbele itakapokua ndo itakapotoa faida kubwa". Amesema

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono mafunzo hayo ili yaweze kuwa na tija kwa wastaafu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba amesema hadi kufikia mwezi Juni, 2021, mfuko ulikuwa na wanachama 705,484 ambao ni watumishi wa Umma na wafanyakazi wa makampuni ambayo Serikali inamiliki hisa zaidi ya 30%.

"Kwa kipindi hicho , mfuko ulikuwa unahudumia wastaafu na wategemezi 188,330". Amesema CPA.Kashimba.

Aidha CPA.Kashimba amesema tangu kuanza kwa mfuko huo Agost 1, 2018 hadi Juni 30, 2021 mfuko umelipa wanufaika 143,367 jumla ya shilingi Bilioni 5,073.Kiasi hicho cha fedha kilitumika vizuri na wanufaika, kinaweza kikatoa mchango mkubwa katika kuendeleza miradi mbalimbali , kutengeneza ajira kwa vijana, kuongeza pato la mstaafu na hatimaye pato la Taifa.

Pamoja na hayo ACP.Kashimba amesema mfuko kwa mwezi Julai 2021 umelipa wanufaika wa pensheni ya mwezi 145,417 yenye thamani ya shilingi Bilioni 56.11.Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Kazi, Ajira,bunge ,Uratibu, Vijana na wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku mbili kwa wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi waa Umma (PSSSF) leo jijini Dar es Salaam.Picha kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Grayson Henry Mwaigombe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, CPA Hosea Kashimba  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku mbili kwa wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi waa Umma (PSSSF) leo jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku mbili kwa wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi waa Umma (PSSSF) leo jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...