Na Karama Kenyunko Michuzi TV

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema, awamu ya pili ya udahili na zoezi la kuthibitisha udahili kwa waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi  ya kimoja katika awamu ya ya kwanza ya udahili ngazi ya shahada ya  kwanza mwaka wa masomo 2021/ 2022 itafungwa rasmi Septemba 6, 2021.

Katibu Mtendaji wa TCU,  Profesa Charles Kihampa amesema hayo leo Septemba 4,2021 wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuelezea  mwenendo wa udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Amesema, mpaka sasa jumla ya  waombaji 31,395  waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kati ya 35,548 wameshajithibitisha kwenye chuo kimojawapo na amewataka wale ambao hawajajithijitisha wakamilishe uthibitisho wao kwenye vyuo wanavyovipenda.
Amesema, baada ya kufungwa kwa awamu ya pili, vyuo vitaendelea na zoezi la kuchakata na kuidhinisha maombi na kisha kutangaza majina ya waliodahiliwa na vyuo husika Septemba 18,2021.

Aidha amesema, Septemba 18 hadi 24,2021 awamu ya tatu ya udahili utafunguliwa hivyo washtakiwa waombaji ambao bado hawajatuma maombi ya udahili mpaka sasa watumie vizuri muda uliobaki kutuma maombi yao kwa usahihi kwenye vyuo wanavyovipenda

"Tume inaelekeza Taasisi za Elimu ya juu kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi na waombaji wa vyuo vikuu pia wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili", amesema Profesa Kihampa.

Aidha Profesa Kihampa amewasisitiza waombaji wa udahili kusoma miongozo ya sifa ya kujiunga na programu husika ili kuona kama wanakidhi vigezo kabla ya kutuma maombi ya udahili,  waombaji wenye changamoto ya kupokea namba ya siri ya kujithibitisha katika chuo kimoja wanaelekezwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ili kupata namba hizo.

Pia Tume inawashauri waombaji kutumia barua pepe ama namba za simu ili kupata urahisi wa kupokea namba za siri, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili, Taasisi zote za Elimu ya Juu zihakikishe waombaji wanajithibitisha wao wenyewe kupitia akaunti zao na si vinginevyo.

Miongozo mingine ni pamoja na waombaji wanaotaka wanaotaka kubadili uthibitisho kuingia katika akaunti za vyuo walivyojithibitisha na wakitaka kubadili maombi yao ya udahili waingie katika akaunti zao za vyuo walivyodahiliwa na kufuta udahili wao ili kutuma upya maombi yao.

"Tume inaelekeza Taasis zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa shahada ya kwanza kuendelea na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo katika zoezi la udahili ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa walazima kwa waombaji udahili na wananchi kwa ujumla" amesema Kihampa.

Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari akielezea masuala mbalimbali ya Udahili katika Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasis (TCU), na  (kulia) ni Mkurugenzi wa uratibu wa Udahili na utunzaji wa Kanzidata wa Time hiyo Dkt Kokuberwa Kulunzi-mollel
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...