WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb)  Septemba 3, 2021 Jijini Dar es Salaam  amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu  na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu  maendeleo ya Sekta ya elimu ikiwemo kuendeleza ushirikiano katika kutoa Elimu bora Nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Ndalichako amesema ni vizuri kuendeleza misingi ya ushirikiano katika masuala ya Elimu ikiwa ni kudumisha Muungano na kwa pamoja kuendelea kutoa wahitimu wenye ujuzi stahiki kulingana na mahitaji ya Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako,  viongozi wengine wa Wizara na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Saidi pamoja na ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ofisi za wizara jijini Dar es Salaam kuzungumzia   masuala mbalimbali ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusu masuala ya elimu yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi alipofika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...