Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani, kimejipanga kuunga mkono kwa asilimia
100, dhamira ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Samia Suluhu Hassan ya
kugombea Urais 2025 na kuhakikisha anashika dola.
Aidha
chama hicho kimepongeza hotuba ya kwanza ya Rais Samia aliyoitoa katika
mkutano wa 76 kwenye Baraza Kuu la Umoja na Mataifa ambayo imegusa
maisha ya watanzania na kulitangaza Taifa kwa uwekezaji na utalii.
Akitoa
maazimio manne ya mkutano wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi
mkoa ,katibu wa CCM Pwani ,Elias Mpanda alisema dhamira ya kushika dola
mwanamke katika uchaguzi mkuu ujao ni wa kuungwa mkono.
Alisema ,wanachama wa CCM wapo sambamba kwa CCM kushinda kwa kishindo ikifika wakati huo.
Pamoja
na hilo ,Elias alieleza Rais Samia tangu ameingia madarakani
ameendelea kudumisha ushirikiano kimataifa na amethubutu kuongea na
wawekezaji na wafanyabiashara na kupanua wigo wa uwekezaji kwa kiwango
kikubwa.
Pia wamehimiza wananchi kupata chanjo ya Uviko 19 kwani ni chanjo salama .
Hata hivyo Elias ,aliwataka wananchi kujiandaa na sensa ya watu na makazi 2022 .
Awali Mwenyekiti wa CCM Pwani, Ramadhani Maneno alisisitiza umoja na mshikamano kwa wanaCCM .
Aliipongeza serikali ya awamu ya sita,kwa kuinua uchumi, maendeleo na kudumisha na kuimarisha demokrasia .
Nae
mkuu wa mkoa wa Pwani , Aboubakari Kunenge akitoa taarifa ya
utekelezaji wa ilani 2020-2025 , alieleza mkoa unatarajia kupata bilioni
314 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji .
"Upatikanaji
wa maji safi na salama umetokana na kukamilika kwa miradi 26
iliyotekelezwa 2019-Juni 2021"Miradi mitano ya bilioni 3.930.685 ni
mipya na miradi 21 inafanyiwa ukarabati kwa gharama milioni 651.502.112
kwa jumla miradi hii itanufaisha wakazi 28,889"
Kunenge
alieleza,bajeti 2021-2022 jumla ya bilioni 17.916.266.5 kupitia mfuko
wa maji program ya lipa kwa matokeo na serikali kuu zimetengwa kwa ajili
ya miradi 94.
Sekta ya maji imekuwa na mafanikio mkoani Pwani kutokana na kufikia wananchi kwa asilimia 72 vijijini na asilimia 84 mijini .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...