Na John Walter-Hanang

Mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja ameungana na wananchi wa kijiji Lambo kata ya Masakta kuchimba mtaro utakaopitisha mabomba kusambaza maji katika eneo hilo na vijiji jirani.

Akizungumza katika zoezi hilo Mayanja alisema kuwa usambazaji wa maji katika eneo hilo lipo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ( RUWASA) Wilaya ya Hanang ambapo alimtaka mkandarasi ahakikishe ndani ya miezi minne kijiji hicho kiwe kinapata maji.

Wanakijiji wa kata hiyo wamesema mkuu wa wilaya kufika katika eneo hilo inawapa matumaini ya kutatuliwa kwa Changamoto ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.

Aidha wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuamua kuungana nao kwa ajili ya kuhakikisha maji yanapatikana ndani ya muda mfupi katika kijiji hicho kwani tangu kuanzishwa kwake upatikanaji wa huduma hiyo ni kwa tabu.

Aidha Meneja wa RUWASA Wilaya ya Hanang Mhandisi Herbert Kijazi amewahakikishia wanakijiji wa eneo hilo pamoja na mkuu wilaya kuwa wafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha usambazaji wa maji katika kijiji hicho ndani ya miezi.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...