Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro amesema ameona ni busara kuendelea na ziara ya kutoa mrejesho wa kero na changamoto za wananchi ambazo tayari mtangulizi wangu Edward Mpogolo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Same alishaziaikiliza
Akizungunza kuhusu mejesho wa kero,Murro amesema wanachokifanya sio kwenda tena kusikiliza kero bali kupeleka mrejesho wa hatua walizochukua katika kuzitatua zile ambazo tayari mtangulizi mwenzake alishazisikilzia maana Serikali ni taasisi na lazima katika nafasi zao waoneshw uwezo wa taasisi na sio uwezo binafsi wa mtu
"Katika kulitekeleza hili, nimepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha kaugeri kata ya Mwaru tarafa ya Sepuka, jimbo la singida magharibi kutoka ikungi mpaka kijiji cha kaugeri kata ya mwaru ni zaidi ya kilometa 350,
"Hapa kulikuwa na changamoto ya umaliziaji wa jengo la Zahanati, nimekwenda sasa kuwapa mrejesho kuwa Rais, Samia Suluhu Hassan ameridhia Sh.milioni 50 zitolewa na tayari tumeshaingiza kwenye akaunti ya kijiji kazi inaendelea.
"Hapa tumefanikiwa kutatua kero ya zahanati sasa malengo yetu ni kuboresha zahanati na kuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kuhudumia wananchi wengi zaidi.Rejea maneno ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga akila kiapo alisema lazima kwenye serikali kuwe na muunganiko wa pamoja (team work) sisi Ikungi tunaitekeleza falsafa hii kwa vitendo sasa,"amesema Murro.
Home
HABARI
DC JERRY MURO KUENDELEA NA ZIARA YA KUTOA MREJESHO KERO NA CHANGAMOTO KWA WANANCHI WA IKUNGI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...