Zikiwa zimebaki siku chache darasa la saba kufanya mtihani wao wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro amewataka viongozi wa Dini na wazazi kufanya maombi ili Wanafunzi wapate ufaulu mzuri.
Wito huo umetolewa na Mkuu huyo wa wilaya wakati wa misa ya shukran ya Fadher Africanus Kanju baada ya kusimikwa kuwa Padre wa kanisa katoriki.
Lazaro alisema Wilaya ya Lushoto imekuwa haifanyi vizuri katika matokeo ya kila mwaka ya darasa la saba hivyo alieleza ni muhimu viongozi wa dini wakafanya maombi ili huyo shetani anayefanya watoto wasifanye vizuri asipate nafasi kipindi hiki.
"Nimeangalia takwimu ya matokeo ya kitaifa ya darasa la saba nikakuta shule nane za mwisho zipo katika wilaya yetu ya Lushoto jamani hii ni aibu na fedheha"Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Alisema kuwa Serikali inatumia rasilimali kubwa na inatoa elimu bure inapaswa walimu wajitoe katika ufundishaji ili kupatikane Matokeo mazuri na hatimaye kama wilaya waondokane katika mnyororo wa kushika mkia.
Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa katika kupambana na matokeo mazuri wameamua kuanzisha makambi katika shule zote za wilaya hiyo lengo ni kuongeza ufaulu katika wilaya ya Lushoto kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...