Tarehe 4 Septemba, 2021, nilipata nakala za kitabu changu kipya Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences. Hima nilimpa nakala jirani yangu, Mama Merri, mwalimu mstaafu anayependa sana kusoma maandishi yangu na ni mfuatiliaji wa shughuli zangu za kuelimisha waMarekani kuhusu utamaduni wa Afrika na tofauti zake na ule wa Marekani. 

Ni bahati njema kwa mwandishi kuwa na wasomaji na wafuatiliaji wa aina ya huyu mama. Lakini kwa hapa Marekani, bahati hiyo ninayo sana. Nina wasomaji na wafuatiliaji wengi.

Mama Merri alifundisha kwa miaka mingi katika shule za waHindi Wekundu. Alivyosoma kitabu changu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences aliandika maelezo kuhusu namna utamaduni wao unavyofanana na ule wa waAfrika nilioelezea kitabu. Ninashukuru kwa elimu anayonipa.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...