Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akichoma jumla ya nyavu haramu themanini (80) za kuvulia samaki katika bwawa la Mtera zenye thamani ya shilingi 13,814,000 katika kijiji cha migoli kata ya migoli
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo amechoma jumla ya nyavu haramu themanini (80) za kuvulia
samaki katika bwawa la Mtera zenye thamani ya shilingi 13,814,000 ambazo zimekamatwa
katika kipindi cha mwezi wa saba 2021 hadi mwezi wa tisa mwa 2021 ambazo
zimekuwa zikitumika katika uvuvi harama katika bwawa hilo.
Akichoma nyavu hizo mkuu wa
wilaya huyo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wavuvi kuvua samaki kwa
kutumia njia harama ambazo zimekuwa zikileta madhara katika kuazaliana na kukua
kwa samaki katika bwawa hilo.
Alisema kuwa sio mara ya kwanza
kuchoma nyavu hizo harama kwenye bwawa hilo la Mtera kwani katika kipindi cha
mwezi wa saba mwaka 2020 hadi mwezi wa nane mwaka 2021 uongozi wa Halmashauri
wa wilaya ya Iringa ulikamata jumla ya nyavu haramu 11,538 zenye thamani ya
shilingi 152,100,000.
Moyo alisema kuwa kwa kipindi
hicho chote wamekuwa wakikamata nyavu aina ya Timba,Kokoro,Gonga,Kimila na
nyavu chini ya nchi tatu ambazo mara
nyingi ndio zimekuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa hilo la Mtera na
kuasababisa uchumi wa wananchi kuyumba kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa
elimu ya usimamizi shirikishi wa kulinda rasilimali za uvuvi na kudhibiti uvuvi
haramu imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa wavuvi ambapo zaidi ya wavuvi 249 na
vikundi 5 vya BMU,wafanyakazi 103 wa samaki wamefanikiwa kupata elimu ya
udhibiti wa usafirishaji wa samaki wachanga kwa mujibu wa sheria ya uvuvi ya
mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.
Aidha Moyo alisema kuwa katika
kuimarisha udhibiti wa wavuvi haramu na ulinzi wa rasimali za uvuvi katika
bwawa la Mtera kwa sasa limekuwa shirikishi na jamii kwa kuunda kikosi kazi cha
kudhibiti uvuvi Haramu kwa kuwa jamii hiyo inawajua wavuvi haramu na ni kazi
rahisi kuwadhibiti chini ya uongozi wa kata,mkuu wa kituo cha polisi migoli na
afisa uvuvi wa kata ya Migoli.
Moyo alimalizia kwa kusema kuwa
lengo la kuunda kikosi kazi hicho ni kulinda samaki waliopo katika bwawa la
mtera ambao ndio wamekuwa wamekuwa tegemeo kwa uchumi wa wananchi wa kata ya
Migoli na maeneo ya jirani hivyo bila mikakati maalumu samaki hao watapotea
katika bwawa hilo.
Kwa upande wake diwani wa kata
ya Migoli Benito Kuyugwa alisema kuwa kutokana na uvuvi haramu kumesababisha
kushuka kwa uchumu wa wananchi wa kata hiyo na baadhi ya wananchi wa kuyakimbia
makazi yao kutokana na sababu za kiuchumi.
Kuyugwa alisema kuwa migori ya
sasa sio ya miaka ya nyuma kutokana na wananchi wake kushuka kiuchumi kutokana
na baadhi ya wavuvi kuvua samaki kwa njia haramu ambazo zimesababisha kupungua
kwa kuzaliana kwa samaki katika bwawa la Mtera na kushusha uchumi wa wananchi
ambao wamekuwa wanategemea uvuvi kuendesha maisha yao.
Kuyugwa alisema kuwa
wamefanikiwa kuunda kikosi cha watu 64 ambacho kitapambana na uvuvi haramu na
kuwakamata wavuvi na zana zao zote ambazo wanazitumia katika kuvua samaki
haramu kwenye bwawa hilo.
Aliiomba serikali kuendelea na
doria za mara kwa mara ili kukomesha uvuvi haramu ambao kwa kiasi kikubwa
umerudisha nyuma maendeleo ya wanananchi wa kata ya migoli na maeneo mengine
yanayolizinguka bwawa hilo.
Kwa upande wake afisa mifugo na
uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa methew Sanga alisema kuwa kwa kipindi
cha mwezi wa saba 2021 hadi mwezi wa tisa mwa 2021 wamefanikiwa kuwakamata
wavuvi kumi na moja (11) na wavuvi tisa (9) wamelipa faini na kuachiwa huku
wavuvi wawili (2) wameshindwa kulipa faini hadi hivi sasa wapo maabusu
wakisubili huku kwa kuwa tayari walikiri makosa yao kwa kukubari kufanya vitendo
hivyo vya uvuvi haramu.
Alisema kuwa serikali imepata
boti moja kwa ajili ya doria ya kuwabaini wavuvi haramu ambao wamekuwa
walivisumbua vyombo vya ulinzi vya bwawa hilo hivyo uwepo wa boti hiyo
kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu katika bwawa hilo la Mtera.
Sanga alimalizia kwa kusema
kuwa serikali ya Halmashuri ya wilaya ya Iringa imetoa elimu kwa viongozi wa
serikali,wavuvi na wasafirishaji 121 kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu kwa
kuzingatia sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanunuzi zake za mwaka
2009 ambapo zinamtaka kila mmoja kufanya biashara wakiwa na leseni za uvuvi na
biashara ya samaki pamoja na matumizi ya nyavu zenye nchi 3 ili kutovua samaki
wachanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...