Na Angela Msimbira TAMISEMI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za  Mikoa na Seriakli za Mitaa Dkt. Festo Dugange amewataka Waratibu wa Maabara wa Mikoa na Halmashauri zote  nchini kuhakikisha wanathibiti upotevu wa bidhaa za afya na kusimamia upotevu wa fedha zinazotokana na utoaji wa huduma za maabara nchini ili zitumike kwenda kununua vitendanishi.

Akifungua kikao kazi cha waratibu wa maabara wa Mikoa na Halmashauri  leo Mkoani Dodoma Dkt. Dugange  amesema katika eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa mapinduzi  makubwa ni kuboresha upatikanaji na matumizi sahihi ya bidhaa za afya vikiwemo vitendanishi vya maabara.

Anafafanua kuwa  idadi ya vitendanishi vya maabara hailingani na idadi ya wagonjwa waliohudumiwa katika vituo vya  kutolea huduma jambo ambalo halileti picha nzuri, kwa kuwa maeneo mengi idadi ya vitendanishi na wahudumiwa bado ni changamoto.

Amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia kwa karibu na kuhakikisha kila bidhaa ya afya inatumika kwa kufuata miongozo na ufanisi unaoendana na mahitaji ambayo yanatakiwa kuonekana katika utoaji wa huduma za afya nchini.

Aidha,Dkt. Dugange amewaagiza wataalam wa maabara kuhakikisha wanaratibu  mapato yanayochagiwa katika sekta ya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini, ni wajibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...