Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
SERIKALI
imesema kuwa mpango wa elimu bila malipo ,hautasitishwa kama baadhi ya
watu wanavyozusha ambapo maneno hayo ni ya uzushi.
Hayo
yalisemwa wilayani Mkuranga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza
na wanafunzi, walimu na wazazi kwenye shule ya Sekondari Mwandege.
Mwalimu
alisema kuwa mpango wa elimu bila malipo utaendelea na hautasitishwa na
wananchi wasisikilize maneno ya uzushi kwani serikali ya awamu ya sita
ya Samia Suluhu itaendelea na mpango huo.
"Mfano
ni wilaya ya Mkuranga kupitia bajeti ya wizara ya elimu imeipatia kiasi
cha shilingi milioni 326 kwa ajili ya shule za msingi na milioni 200
kwa shule za sekondari kwa ajili ya mpango huo," alisema Mwalimu.
Alisema
kuwa hadi Julai mwaka huu kiasi cha shilingi milioni 114 tayari
zimeshatolewa kwa ajili ya mpango huo wa elimu bila ya malipo kwa wilaya
hiyo.
"Wanasema elimu
bure chini ya Samia itakufa wanaosema hivyo washindwe na walegee kwani
jambo kama hilo halipo ambapo serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili
ya mpango huu,"alisema Mwalimu.
Aidha
alisema serikali itatoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili
ya ujenzi wa shule za sekondari mbili ambapo fedha zinazotolewa ni
shilingi milioni 600 kwa kila jimbo nchini.
"Tumeona
shule hii ina wanafunzi wengi na tumeona shule hii iko jirani na Dar es
Salaam na wengi wanatoka huko serikali itatoa fedha nyingine kwa ajili
ya ujenzi wa shule ya sekondari hivyo mtapate shule mbili," alisema
Mwalimu.
Katika hatua
nyingine ameunga mkono ujenzi wa stendi ya kisasa kwa ajili ya mabasi
yanayokwenda mikoa ya Kusini kwani mabasi hayo kwa stendi ya Mbagala
inakuwa imezidiwa.
Alisema
kuwa hata barabara ya mwendokasi iishie hapo ili kuipunguzia stendi ya
Mbagala wingi wa magari ambapo mabasi hayo hayana stendi maalumu na hapa
stendi iitwe Samia Suluhu Hassan.
Awali
mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa wamedhamiria
kuongeza wigo wa kukusanya mapato kwani ndiyo yanayofanya mambo ya
maendeleo yafanyike.
Kunenge alisema kuwa wamedhamiria kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kutatua changamoto kwenye mkoa ili ibaki historia.
Naye
mkuu wa wilaya ya Mkuranga Hadija Ally alisema kuwa wilaya imetenga
eneo lenye ukubwa wa hekari 11,700 Mbezi kwa ajili ya uwekezaji.
Ally
alisema kuwa wanatarajia kuboresha wa hospitali ya wilaya kuwa kituo
cha afya ili kukabiliana na wingi wa wagonjwa pamoja na kuomba kujengwa
kituo cha afya Mwandege.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...