Na John Mapepele, Dsm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 18,2021 ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuboresha Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite ili liwe miongoni mwa vivutio vya utalii na kuliingizia taifa mapatio.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Mhe, Jenista Mhagama jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Tamasha la kwanza la Michezo ya Wanawake la Tanzanite lililobeba kauli mbiu isemayo “kusherekea mafanikio ya wanawake katika michezo” amesema utalii wetu umejikita zaidi kwenye maliasili pekee hali ambayo inawafanya wageni wakitembelea wasirudi tena.

“Michezo ni chombo chenye nguvu katika kutangaza utalii wa nchi, mtakumbuka hivi karibuni wakati nikipokea kombe ya timu ya Taifa chini ya miaka 23 nilieleza umuhimu wa michezo katika kujenga umoja na uchumi na diplomasia ya nchi yetu”. Imefafanua sehemu ya taarifa hiyo

Amesema nchi mbalimbali ambazo zimekuwa zikiratibu mashindano ya kimataifa kama Olpympic zimenufaika na mapato yanayoletwa kutokana na michezo hiyo.

Pia ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuboresha michezo ya jadi kama rede, mdako, mbio za magunia ambapo amesema ina nafasi kubwa katika kushinda kwenye mashindano ya kimataifa.

Akitolea mfano amesema medali ya kwanza ya kimataifa ililetwa nchi na mwanamke mwaka 1965 kwenye mchezo wa kurusha mkuki katika mashindano ya All African games ambapo amesema imekuwa ni nadra kusikia akitajwa kwa jambo hili.

Aidha Serikali imejipanga kuendeleza jitihada za awali za kukuza michezo ndiyo sababu aliamua katika siku za hivi karibuni kuitoa Idara ya Habari katika Wizara hii ili kuendeleza michezo nchini.

Ametoa wito kwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuangalia mapato ya matangazo kwenye uwanja wa Mkapa na kusimamia maslahi ya wachezaji ambapo amesisitiza kuwa kukiwa na na utamaduni wa kulea vipaji kuanzia chini kama ilivyo kwenye UMISSETA na UMITASHUMTA kutasaidia  kukuza  michezo.

Amesema kwa sasa tayari Serikali imeshatenga  kiasi cha shilingi bilioni1.5 kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Michezo, na inatarajia kujenga ukumbi wa kisasa wa michezo ili kuboresha michezo ambapo ametoa wito  kwa wazazi kuwasisitiza Watoto kutilia maanani elimu na kushiriki kwenye michezo.

Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema Tamasha hili limepewa jina la Tanzanite kutokana na umuhimu wa wanawake ambao umefananishwa na madini yenye thamani ya Tanzanite

Akitoa salamu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegero amesema Tamasha hili limetoa hamasa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao kupitia ambapo ameiomba Wizara kuendelea kuratibu matamasha mbalimbali kama hili la Tanzanite kwa ajili ya kuendeleza michezo.

Mwenyekiti wa Tamasha la Tanzanite, bibi Neema Msita,amemshukuru Mhe. Rais kwa maono yake katika kukuza michezo ya wanawake nchini.

“Katika kipindi kifupi ameweza kubeba maono ya kimapinduzi na kubeba ajenda ya wanawake katika nyanja mbalimbali. Amesisitiza Msita

Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Solo Mwamba na Nandy wamekonga nyoyo za wanamichezo na wadau mbalimbali wa michezo kwenye uzinduzi wa tamasha la kwanza la michezo

Tamasha hili lilikuwa la siku tatu kuanzia Septemba 16-18, 2021 ambapo siku ya kwanza ilianza na kongamano lililojadili maada mbalimbali za michezo ambapo siku ya pili na tatu zilifunikwa na michezo mbalimbali iliyotoa hamasa kubwa kwa wadauwa michezo na wananchio kwa ujumla.

Miongoni mwa michezo iliyochezwa ilijumuisha soka, riadha, wavu, kikapu, karate, michezo ya jadi, (kuruka Kamba, Rede na ngoma) na kutunisha misuli.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...