Charles James, Michuzi TV
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi, Jerry Silaa wa Ukonga na Josephat Gwajima wa Jimbo la Kawe wote wa Mkoani Dar es Salaam wamefika katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM.
Wawili hao wameripoti muda tofauti asubuhi ya leo ikiwa ni kutii agizo la kuitwa na kamati hiyo lililotolewa jana na Katibu wa Kamati, Rashid Shangazi.
Kikao hicho kinaketi chini ya Mwenyekiti wake, Hassan Mtenga ambapo Wabunge hao watahojiwa juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...