Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KLABU ya Simba imesema jezi zake mpya za msimu wa Ligi Kuu Tanzaia bara mwaka 2021/2022 tayari zipo kwenye maduka yote ya Vunja Bei nchi nzima huku ikitangaza pia viingilio vya Simba Day inayofanyika Septemba 19 mwaka huu.

Akizungumza leo asubuhi Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema jezi zote za klabu ya Simba zi zinapatikana kwenye maduka yote Vunja Bei na hiyo imetokana na mahitaji makubwa ya mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba waliko ndani na nje ya nchi kuzihitaji.

"Mashabiki wanahitaji sana jezi hivyo uongozi wa Simba na Vunja Bei umeona hauwezi tena kusubiri hadi zizinduliwe rasmi, presha imekuwa ni kubwa sana ,sasa rasmi jezi za Simba zinapatikana leo kwenye maduka yote ya Vunja Bei na uzinduzi uko pale pale,"amesema na kuongeza" Nimepigiwa simu na Athuman Machupa mchezaji wa zamani wa Simba anayeishi Swiden akiulizia jezi za Simba".

Kamwaga amesema uongozi wa Simba umempa maelekezo Vunja Bei kuhakikisha jezi hizo zinasambazwa madukani na kuanza kuuzwa mara moja huku akitumia nafasi hiyo kutangaza kauli mbiu ya Simba kuelekea Simba Day 2021 inayosema "One Team One Dream " wakiwa na maana Mashabiki wa Simba tuko pamoja ,tuna ndoto moja, na sote tunajua wapi tunataka kwenda,hivyo amewaambia Asubuhi tu twendeni wenye nchi.

Kuhusu viingilio katika Simba Day amesema vipo vya vinne ambavyo ni mzunguko Sh.5000, VIP C na B Sh.20,000 , VIP Sh.30,000 na Platnum Sh 200,000."Kwenyeplatinum unapata jezi mpya ya Simba, chakula kizuri, msafara utaongozwa na Polisi kutoka watakaondokea kwenda uwanjani,watakuwa na sehemu maalum ya kukaa , usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na kupewa kofia za Simba "

Ameeleza kuwa kwa taarifa hiyo tikezi zinaanza kuuzwa leo na hata unapoingia kwenye mtandao unaweza kununua tiketi yako ,lengo ni watu siku ya Simba Day watu wasijazane milangoni, kwani wanataka kuona hakuna usumbufu wa kuingia uwanjani.

"Kwa mtu atakayenunua tiketi yoyote na kwenda kununua jezi dukani atapata punguzo maalum na katika kuelekea Simba Day kuna matukio mbalimbali yatakuwa yakiendelea na taarifa zaidi zitawekwa kwenye mtandao kupitia Simba App, awamu ya pili ya pre season yatawekwa huko huko,"amesema Kamwaga.

Akizungunzia kuhusu kuvuja kwa jezi zao mpya amesema hana uhakika na hizo jezi kwani hajazionq huku akiwomba waandishi wa habari mambo ya aina hiyo kwani yanarudisha nyumq juhudi za kukuza mpira wa Tanzania kiuchumi.

Amesema ameona baadhi ya watu wanashabikia kuvuja kwa jezi lakini wanasahau Simba kuna mwekezaji ambaye ni Vunja Bei ambaye amewekeza Sh bilioni mbili na hiyo ni biashara hiyo ni kubwa nchini, watu wameajiri watu ,hivyo kushabikia jezi kuvuja sio uungana,hakisaidii na kinawapa hasara watu ambao wamamua kuweka fedha zao kwenye biashara ya mpira.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...