Na Khadija Seif, Michuzi TV
WATANZANIA wameshauriwa kujenga uelewa kuhusu tatizo la usonji kwa watoto ili kutengeza uhusiano mzuri na watoto wenye tatizo hilo kwa lengo la kuwasaidia katika masuala mbalimbali yakiwemo kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.
Ushauri huo umetolewa leo Septemba 30 mwaka huu na Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Dk.Said Kuganda wakati wa semina ya kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusiana na tatizo hilo.
Ambapo amesema jamii ya watoto wenye usonji wamekuwa na wakikutana na changamoto kutokana na kuzungukwa na watu wasio na uelewa wa tatizo hilo hali inayopelekea wakati mwingine kutengwa bila sababu.
Ameongeza kutokana na hilo, imekuwa shida kwao kupata matibabu ambayo kama jamii wakiwemo baadhi ya wazazi wangekuwa na elimu juu ya tatizo hilo wangeweza kuwasaidia katika makuzi yao.
" Chanzo cha tatizo hilo hakijajulikana, zaidi imeonyesha kuwa wanaopatwa na usonji akili zao hushindwa kutengeneza mahusiano na jamii inayomzunguka na wakati mwingine kuwa na tabia za kujirudia rudia" amesema Dk.Kuganda."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya 'Lukiza Autism Foundation' iliyoandaa semina hiyo, Hilda Nkabe amesema tatizo la usonji ambalo zaidi kuonekana kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, linahitaji kutolewa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuleta mabadiliko.
Aidha,Nkabe amefafanua kimsingi mtoto mwenye usonji huwa na dalili zinazotofautiana na hivyo wakati mwengine kumsababishia mtoto mwenye tatizo hilo kufanya vitendo vya kumkwaza mtu mwingine jambo ambalo huitaji ukaribu na uelewa wa watu walio karibu naye.
Na katika kujenga uelewa kwa jamii kuhusu tatizo hilo, taasisi yake imeandaa hafla maalumu inayotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itatumika kutoa elimu na hivyo kuondoa hali ya sintofahamu katika jamii.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Dk.Mengi Foundation (DRMF) Shimimana Ntuyabaliwe ameeleza kuna haja kwa jamii kutanguliza utu wakati wa kutamka majina ya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuweka usawa.
Daktari Bingwa wa afya na Magonjwa ya akili wa hospitali ya Taifa Muhimbili,Said Kuganda akifafanua zaidi katika semina iliyowajumuisja Waandishi Wahabari pamoja na wataalam wa afya ya akili,kuwa Kuna haja ya jamii kupewa Elimu ya uelewa kuhusu Magonjwa ya akili
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Autism akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kutoa semina kwa Waandishi Wahabari jijini Dar es salaam huku akiwataka jamii kuelewa jinsi ya kuwasaidia watoto wenye Matatizo ya akili (Usonji)
Baadhi ya sehemu ya Waandishi Wahabari wakisikiliza kwa umakini semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Lukiza Autism Foundation
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...