Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima kizungumza katika mkutano wa Mashirika yasiyo ya kiserikali leo Jijini Dodoma ambapo uliambatana na semiana elekezi kwa watendaji na wadau wa mashirika hayoWashiriki na wamiliki wa NGOs wakiwa katika mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma leo.29/30/2021.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakiwa katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Mkutano ukiendelea katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete leo Jijini Dododma ambapo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima.


Na.Vero Ignatus,Dodoma

Mkutano mkuu wa mwaka Mashirika yasiyo ya kiserikali unaofanyika jijini Dodoma ukiwa umebeba kauli mbiu isemayo "kuimarisha mchango wa NGOs katika maendeleo ya Taifa" ,umeshirikisha wadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar


Akitoa salamu kwa mgeni rasmi muwakilishi wa NGO Bungeni Neema Lugangira alisema kuwa anaiomba serikali kupitia wizara ya afya kuangalia vyema suala la kanuni mpya za NGO kwenye eneo ambalo linataka kabla ya kufanya kazi yeyote kwamba NGO inatakiwa kupata kibali kutoka hazina wizara ya fedha jambo ambalo linachelewesha utekelezaji wa kazi za taasisi husika,kwani wakati mwingine mradi huo unatakiwa kutekelezwa ndani ya miezi sita.

Nashukuru sana kamati ya bunge ya sheria ndogo waliridhia ombi hilo na walitoa maelekezo kwamba wizara iweze kupitia mapendekezo hayo,kipekee nimshukuru sana Spika wa Bunge Job ndugai ambae alikazia umuhimu wa kufanya mapitio ya kanuni hizi kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira wezeshi kwa ajili ya ustawi wa taasisi husika,hivyo ni matamanio yangu katika mkutano huu tutapata mwelekeo wa lini kipengele hiki kitapata maboresho ili kiletwe bungeni ili na sisi tuweze kufanya uchakataji na kufanya kazi husika.alisema Neema

Aidha alitoa ombi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba alipokuwa kwenye mkutano wa 76 wa baraza kuu la umoja wa mataifa alielezea dira yake na dhamira yake kwamba tunaongeza nafasi za wanawake kwenye uongozi usawa wa kijinsia na kufikia 50 kwa 50 na jambo hili amakekuwa akilisema mara nyingi

Hivyo ni ombi langu kwa mhe.Rais kwamba tufanye mapitio ya na maboresho ya kanuni za uchaguzi ndani ya ccm na katiba ya CCM ili kuwepo na kipengele kinachoelekeza ya kwamba katika nafasi za wagombea asilimia 30% ya wagombea wawe ni wanawake.

"Mashirika haya yamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo tunayojivunia ya Taifa la Tanzania" alisema Neema.

Hata hivyo ametoa wito kwa mashirika hayo kufanya kazi kwa Ueledi ,Uadilifu pamoja na upande wa serikali uimarike katika kufanya kazi kwa weledi,

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wajumbe wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amempongeza mbunge huyo kwa jitihada kubwa alizozifanya kwa nafasi yake bungeni, kwa lengo la kuimarisha utendaji wa Asasi za Kiraia kwa kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji hali inayoonekana kubadili mwelekeo wa utendaji kazi

Akifafanua juu ya masula ya Kodi Bwana Matenus Mallya, amesema Mamlaka ya mapato Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia, wamekuwa wakichangia Pato kubwa Serikalini isipokuwa wengi wamekuwa hawatambui ni mapato yapi wanapaswa kuchangia, mchango mkubwa wa asasi za Kiraia inakwenda moja kwa moja katika ngazi ya Jamii na kupelekea kuongezeka kwa idadi kubwa ya walipakodi wa hiyari.

Kupitia mfumo wa ulipaji Kodi, na usajili wa mlipa Kodi, kwa kila Taasisi ili kuweza kukidhi vigezo ili Asasi zinazofikia muzo ghafi ya zaidi ya 14 milioni kuweza kusajiliwa kwa kupata EFD mashine.

Kuhusu ombi la Charitable status, Bwana Octavian Machenje vigezo anavyotazama Kamishina wa mapto, kinatokana na Sheria ya Kodi ya mapato katika kifungu Cha 64, ambapo Sifa muhimu ni, maudhui ya Katiba, shughuli zinazofanyika katika taasisi pamoja uwanda wa kazi unazozifanya katika taasisi husika.

Akizungumza Utaratibu wa kuingia Nchini kwa wageni wanaokuja kufanya kazi za NGO bwana Amon Kamoga amesema Sheria imeweka utaratibu wa vibali vya mda mfupi kwa siku 90 (visa au Pasi) na muda mrefu kwa zaidi y siku 90 kibali cha ukazi kwa kuangalia vigezo vya shughuli unayokuja kufanya kazi nchini, pamoja na mtu mwenyewe anyeomba kibali kutokana na mahali anapotoka.

Aidha wajumbe wa mkutano wanatarajiwa kukutana na mh Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atahutubia mkutano huo wa siku mbili ulioanza na semina elekezi kwa katika masuala mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...