Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeipiga msasa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwa kuipatia mafunzo maalumu yenye malengo mbalimbali hasa maslahi ya Taifa.

Pamoja na mambo mengine, mafunzo hayo pia yatajikita katika masuala ya Itifaki, mawasiliano ya Kidiplomasia, usalama wa Kimtandao na Diplomasia ya Uchumi ili kuwajengea uwezo wabunge wa kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yao ya Kamati na Bunge kikamilifu.

Akifungua mafunzo hayo ya siku tano Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa kupitia mafunzo hayo kamati itapata ujuzi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Kamati maslahi ya Taifa, masuala ya Itifaki, mawasiliano ya Kidiplomasia, usalama wa Kimtandao na Diplomasia ya Uchumi ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yenu ya Kamati na Bunge kikamilifu.

“Ninayo furaha kuwajulisha kuwa mtapata fursa ya kuelimishwa juu ya mambo Uchumi wa Buluu, mada itakayotolewa na Wizara yenye dhamana ya usimamizi wa uchumi wa buluu kutoka Zanzibar ambayo imepiga hatua katika utekelezaji wake,” Amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Wizara inaamini kuwa wajumbe wa Kamati na washiriki wote wa mafunzo wataendelea kutumia ujuzi watakaoupata kuishauri Wizara na kuwa Mabalozi wazuri ndani na nje ya Bunge katika kulinda taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Niihakikishie Kamati kuwa Wizara itaendelea kushirikiana nanyi kikamilifu hasa katika kipindi hiki tunapoandaa Sera yetu ya Mambo ya Nje. Tunaamini kuwa ushiriki wenu utaiwezesha nchi yetu kuwa wa sera iliyosheheni masuala muhimu yatakayoiwezesha nchi kunufaika,” ameongeza Balozi Mulamula

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Bw. Mussa Zungu (Mb) amesema kamati anayoiongoza inafanya kazi kuwa kwa maslahi mapana ya nchi na kuahidi kuwa vichocheo vya maslahi ya nchi vinalindwa kwa maslahi mapana ya nchi.

“Kamati inatoa ushauri ‘cross-cutting’ kwa maana inagusa kila eneo kwa taifa letu, jambo lolote lile linalohusiana na masuala ya foreign huwa tunashauri, mambo ya ulinzi na usalama,kwa hiyo inatoa mambo yak echini kwa chini kwa malengo ya kuisaidia serikali,” Amesema Bw. Zungu

Mafunzo haya muhimu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Chuo cha Diplomasia na yatafanyika kuanzia leo tarehe 13 – 17 Septemba 2021 jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Bw. Mussa Zungu (Mb) Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) hayupo pichani

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi. Agnela Nyoni akitoa hotuba kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuongea na wajumbe wa Kamati ya NUU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba ya ufunguzi wa mafunzo maalum ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...