Girl Guides wakiimba na kucheza wakati wa ufunguzi wa Kambi ya mafunzo elekezi kwa viongozi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo yanashirikisha viongozi kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani.
Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Maembe akizungumza alipokuwa akifungua kambi ya mafunzo kwa viongozi wa TGGA, Kulia kwake ni Kamishna Mkuu wa TGGA,Symphorosa Hangi na Mwenzekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro.TGGA imetimiz.a miaka 93 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Anna Maembe (kulia) Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (katikati) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa TGGA,Symphorosa Hangi akiwasalimia viongozi na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo ya mafunzo..
Kamishna Mkuu wa TGGA,Symphorosa Hangi akiwasalimia viongozi na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo ya mafunzo..
Mmoja wa viongozi wa TGGA kutoka Zanzibar akiburudisha washiriki kwa kuimba utenzi.
Skauti wakipita kujitambulisha.Kamishna msaidiyi Mkuu wa TGGA, Sara Milunga (katikati) akiwa na Kamishna Mkuu, Symphorosa (kulia) pamoja na mgeni rasmi, Anna Maembe.PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video Mgeni rasmi Anna Maembe akihutubia baada ya kusikiliza risara ya viongozi wa TGGA wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo.....



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...