Wakati maonyeso ya Madini yakiendelea mkoani Geita wachimbaji wadogo wamelamba bingo kwa kuingia mkataba wa ushirikiano kibiashara na kampuni ya uuzaji wa mitambo ya kuchimbia madini na magari ya mizigo ya GF Trucks & Equipment’s Ltd
Ikionekana kuguswa na kauli ya Waziri mkuu Kassimu Majaliwa aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Maonyesho hayo mkoani Geita aliwataka wawekezaji kuwakopesha au kuwapatia mikopo nafuu ya Mashine au mitambo ya kufanyia kazi migodini badala ya pesa kitu ambacho kwa mchimbaji sio kipaumbele
Kwa kuzingatia hilo kampuni ya Gf inayouza Mitambo ya migodini ya XCMG pamoja na magari ya mizigo ya FAW imeingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja na Umoja wa wachimbajin madini Wadogo wadogo mkoani Geita (GEREMA.)
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo GEREMA Mkurugenzi wa Kampuni ya Gf, Salman Karmal alisema Kutokana na kampuni hiyo kujikita katika uuzaji wa mitambo ya migodini na wadau wakuu ni wachimbaji wadogo na wakati basi kampuni ikaona kuna haja ya kuingia mkataba wa kindugu baina na GF na GEREMA
Leo hii tunafugua ukurasa mpya kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kufanya kazi pamoja na wachimbaji wadogo wa madini ambao ni wanachama wa (GEREMA) hapa Mkoa wa Geita.
Kupitia mkataba huu utamwezesha Mwanachama wa Umoja wa wachimbaji kuingia katika familia ya ya GF na itamwezesha kupata mkopo wa mitambo na maroli, bila kuwa na mashariti magumu, wala riba, sifa kubwa itakuwa ni yeye awe katika Chama hicho tu.
Tunajua wachimbaji wadogo hawana uwezo wa kununua mitambo ya kuchimbia ili kukidhi mahitaji kwa kulitambua hilo kuanzia leo wachimbaji hao wadogo wanaweza kukopeshwa Mitambo ,Magari kwa vigezo vidogo ambavyo hapo awali walikua hawana uwezo huo.
Baada ya kuingia kwenye makubaliano ya ushirikiano kati ya Gerema na GF Truck ,Katibu wa chama cha wachimbaji wadogo mkoani hapa Golden Hainga alisema mpango huo utaleta manufaa na tija kwa wachimbaji ambao hawana mitaji hivyo kufanya kazi kwenye mazingira magumu yasiyo na tija na wakati mwingine kupata hasara.
“Utaratibu huu wa GF Truck ni mkombozi kwa mchimbaji mdogo maana hawa wataweka dhamana na benki itatoa fedha ,wachimbaji wamekua na kilio miaka mingi wakiomba kukopeshwa vifaa au fedha ujio wa hawa wadau utasaidia hata mabenki kuwa na imani na wachimbaji”alisema Hainga.
Pia Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa makubaliano hayo alisema lengo la maonyesho ya madini ni kuwakutanisha wachimbaji na wadau mbalimbali ambao kwa njia moja ama nyingine watajenga ushirikiano baina yao na wachimbaji .
Aidha aliwataka wachimbaji wanaopatiwa mkopo kurudisha kwa wakati ili kujenga imani kwenye taasisi za fedha ambazo hadi sasa zinahofu ya kuwaamini wachimbaji wadogo na kuwapatia mkopo pia aliwakaribisha GF na wadau wengine kuwatembelea Wachimbaji wadogo ili kutambua changamoto wanazokaliliana naza na kuwasaidia .
Mkuu wa mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule(katikati) akishuhudia ubadilishanaji nyaraka kati ya Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd,Salman Karmal(kushoto)na Katibu wa chama cha wachimbaji wadogo mkoani Geita(GEREMA) , Golden Hainga baaada ya kusaini makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya GF na GEREMA wakati wa maonyesho ya Madini mkoni Geita .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...