
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakwanza kulia akiwa na wenzake watatu wakiwa katika mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Mafisadi jijini Dar es Salaam leo Septemba 16,2021.

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Freeman Mbowe na wenzake watatu imeshindwa kuendelea kusikilizwa kwa wakati uliopangwa kutokana na taratibu zilizowekwa na Mahakama.
Baadhi ya taratibu hizo ni kuzuia wafuasi wa Chadema kuingia na simu katika ukumbi wa Mahakama utaratibu ambao unapingwa na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala.
Kesi hiyo ambayo leo Septemba 16,2021 ilikuwa inakuja kwa ajili ya shahidi wa upande wa Jamuhuri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhani Kingai ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi na kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kuhojiwa na mawakili wa upande wa huo kufuatia upande wa utetezi kumaliza kumuhoji shahidi huyo, (Re Examination) ilipangwa kuanza kusikilizwa saa nne asubuhi ya leo lakini mpaka mchana wa saa sita ilikuwa bado haijaanza.
Wakati wadau mbali mbali wa Mahakama wa wakiwa wameishaingia kwenye ukumbi wa wazi wa mahakama kwa wakisubiri kesi kuanza kusikilizwa, karani wa mahakama hiyo alitoa Tangazo la kuwataka watu wote watoke nje ya ukumbi huo wa wazi na kuwaacha watuhumumiwa ndani.
Hata hivyo muda mfupi baada ya wadau hao kutoka nje, watuhumiwa nao walitolewa na kurudishwa katika mahabusu ya mahakama hiyo.
Aidha muda mfupi baadae wa watu wote wakiwemo wanaabari walizuia kuingia na simu mahakamani humo.
Mpaka sasa wadau wa mahakama hao wako nje wakisubiri kujua hatma ya usikilizwaji wa kesi hiyo.
Ikumbukwe kuwa, jana Septemba 15, 2021 upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wao Peter Kibataka kupinga mahakama isipokee maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adam Kusekwa yaliyopaswa kutolewa mahakamani hapo kama kielelezo na shahidi wa kwanza wa upande wa Mashtaka, Kingai.
Wakidai kuwa mshtakiwa kabla ya kuchukuliwa maelezo hayo ama wakati akichukuliwa maelezo aliteswa na pingamizi la pili ni kwamba maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...