Katikati ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Ndg. James Kibamba wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Tughe  ndg. Mtani Songwalwa,Wa kwanza kulia ni Naibu katibu wa Baraza Ndg. Adamu Muchuzi pamoja na Ndg. Alquine Masubo ambaye ni Mwakili wa Baraza Kuu Serikalini
Naibu mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya wakili mkuu wa serikali Dkt.Boniphace Nalija Luhende akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya mkutano mkuu uliofanyika Jijini Arusha.
Naibu mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya wakili mkuu wa serikali Dkt.Boniphace Nalija akiwasili katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano AICC kwaajili ya Mkutano Mkuu wa kwaanza wa mwaka wa fedha 2021/22
Katibu wa Tughe tawi la Wakili mkuu wa Serikali wajumbe wa Baraza la wafanyakazi tawi la ofisi ya wakili mkuu wa serikali wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe Baraza la wafanyakazi Tawi la Ofisi ya wakili mkuu wa serikali wakiwa katika kikao Cha kwanza Cha mwaka wa fedha 2021/22
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kile kinachoendelea katika kikao hicho kioichofanyika katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano AICC ukumbi wa Kalolo Jijini Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha

Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali imeweza kuiwakilisha vyema serikali kwa kwenye mashauri ya madai na usuluhishi , hivyo kuweza kuokoa fedha ambazo zingelipwa kwa wadai kiasi Cha Tsh.540,398,775,272.70,wakati upande wa mashauri ya usuluhishi kiliokolewa kiasi kilichookolewa ni tsh,685,474,629 na dola za kimarekani 1,152,572,523,41,hivyo kiliokolewa kiasi cha tsh,bil.541 na dola za kimarekani  mil 1.1, kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Hayo yamesemwa Dkt.Boniphace Nalija Luhende katika kikao cha kwanza Cha Baraza la wafanyakazi ofisi ya wakili mkuu wa serikali kilichofanyika hivi karibuni Jijiji Arusha,ambapo OWMS imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi,kwa kushiriki katika utatuzi wa haraka wa migogoro inayohusu Serikali na washiriki wake ,wananchi au taasisi za Serikali/binafsi,umiliki wa ardhi,kodi,madai ya kikatibana haki za binadamu.

Luhende alisema kuwa Ofisi hiyo  ilimeweza kushiriki vyema katika majadiliano na wadai /wadaiwa wa nje ya mahakama kwa lengo la kumaliza mashauri yaliyofunguliwa na serikali nje ya Mahakama,na kuweza kumaliza mashauri kadhaa ikiwa ni pamoja na shauri la kampuni ya Vodacom Tanzania PLC,ambapo yaliweza kuiingizia serikali kiasi cha tsh.6,645,228,310.10

"OWMS hutumia njia ya usuluhishi ,majadiliano,na kufungua kesi mahakamani,kwa mashauri hayo kuisha kwa wakati kunarejesha Imani kwa upande husika na kuzifanya kuendelea na shughuli za maendeleo.Alisema Luhende

Aidha katika eneo la rasilimali watu Ofisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala Bora, imeendelea kujaza nafasi mbalimbali za watumishi kutoka watumishi 2 (2018)hadi kufikia watumishi 144(2021) kwa lengo la kuongeza ufanisi 

"Juhudi za kuongeza watumishi.zaidi ili kufikia ikama ya ofisi ambapo matarajio ninkuwa na watumishi 312 zinaendelea na tyaari ofisi ya Raise Utumishi wa Umma imeahidi kuendelea kuoitia watumishi kwa mwaka huu wa fedha 202/22.alisema Luhende.

Luhende ameainisha changamoto katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2021/22 upungufu wa watumishi,kwani mahitaji ya ofisi nikuwa na jumla ya watumishi 312,lakini Sasa wapo 144 Kati yao 88 Ni mawakili wa serikali,makatibu Sheria 13 na watumishi wa kada nyingine wapatao 43,hivyo upungufu ni 168,hivyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora jitihada za kuwapt watumishi hao zinafanyika.

Changamoto nyingine ni Upungufu wa watumishi wenye ustadi Maalum,Ufinyu wa Bajeti,kutokuwa na muundo wa Utumishi wa Ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali,Uoungufu wa magari kwani yanayohirajika angalau 35 kwasasa yapo 18 Upungufu 17 hali inayosababisha changamoto nyingi haswa kwenye ofisi za mikoani ambapo ni mikoa 2 Kati ya 15 yenye magari.

Mwenyekiti wa Tughe  ndg. Mtani Songorwa alisema kuwa Baraza la wafanyakazi mahali pa kazi matunda yameanza kuonekana kwa wafanyakazi kushirikishwa katika uandaaji wa nyaraka mbalimbali ,kama vile bajeti ya kila mwaka,mpango kazi ,mpango mkakati wa miaka mitano 2021/2026 pamoja na kushirikishwa kutoa maoni ,kuwasilisha changamoto na kuzipatia ufumbuzi.

"Kupitia vikao mbalimbali vya Idara vikao vya wafanyakazi wote pamoja na vikao vingine vya kisheria Kama Baraza la wafanyakazi Kama ilivyosasa ,moja Kati ya madhumuni ya Mkutano huu ni kiwawezesha wafanyakazi kupitia utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22"Alisema Songorwa.

MWISHO




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...