Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GF Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoni Pwani kimetoa msaada wa madawati na vitanda kwa watoto yatima wanaolelewa na Taasisi ya elimu ya Wipahs lengo likiwa ni kuwasaidia watoto hao lakini kurudisha sehemu ya faida katika Jamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa GFA Imrani Karmali amesema wakati kiwanda hicho kikisherehekea mwaka mmoja tangu kianze kuunda na kuzalisha magari wameona ni vema wakatoa msaada kwa jami
Naye Meneja wipahs, Jabbir Rajan mbali na kushukuru amesema ipo haja kwa taasisi ama kampuni kuiga mfano huo kwa kurudisha sehemu ya faida kwa jamii kwani kwa kufanya hivyo inasaidia kupunguza makali ya kuwahudumia watoto hao.
Meneja mkuu wa kiwanda hicho Ezra Mereng amesema kiwanda kimeendelea kukua na kwa sasa asillimia 95 ya wafanyakazi ni watanzania hii ni baada ya kupewa mafunzo mbalimbali kwa mwaka mzima na watalamu kutoka nchi mbali mbali zenye teknolojia mzuri katika utengenezaji wa Magari,Pia aliongeza kiwanda hicho kipo katika eneo la kibaha hivyo pia kimetoa upendeleo maalumu kwa wakati wa eneo wenye ujuzi ikiwa kama kipaumbele kwao.
Mbali na kutoam misaadfa hiyo kwa wenye mahitaji pia kulifatiwa na tamasha kubwa la michezo ikihusisha wafanyakazi wa kampuni ya GFA pamoja na kampuni mama ya GF Trucks & Equipment katika mpira GFA waliwabugiza wapinzaniao bao 2-0.
wakiomba dua kabla ya kuanza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...