Na Mwandisho wetu
Dar es Salaam. Jumla ya klabu tisa (9) ziashiriki katika mashindano ya wazi ya klabu bingwa ya Taifa yalyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana Septemba 25 na 26.
Klabu
hizo ni, Dar es Salaam Swim Club,
Taliss, Champions Rise, Mwanza Swim Club na Arusha Swim Club pia kuna klabu za Mis
Piranhas, Bluefins na, FK Blue Marlins kwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati
ya maandalizi ya Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Khadija Shebe.
Shebe alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji wenye umri kuanzia miaka tisa (9) na wenye miaka 15 na zaidi katika mashindano hayo yaliyodhaniwa na Samsa Logistics Limited, Sapphire Court Hotel limited, Selcom Paytech ltd, Pepsi, Azam, Gymkhana Club, Tarmal Industries ltd, Tanpack na Flames Restaurant.
Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la miaka tisa na 10, 11 mpaka 12, 13-14, na 15 ambapo muogeleaji atakayeibuka wa kwanza atapata pointi 20 ambapo wa pili na tatu watapata pointi 16 na 14 kila mmoja.
“Waogeleaji watakaomaliza katika nafasi ya nne watapata pointi 12 ambapo wa tano, sita, saba, nane, tisa na 10 watazwadiwa pointi 10, 8, 6, 4, 2 na moja. Haya ni mashindano ya TSA na yapo kwenye kalenda ya chama, hivyo waogeleaji wenye vigezo wanatakiwa kushiriki katika mashindano haya,” alisema.
Alisema kuwa jumla ya staili tano za kuogelea zitashindaniwa katika mashindano hayo ambazo ni backstrokes, butterflies, individual medleys, breaststrokes na freestyles.
“Tunawashukuru wadhamini ambao mpaka sasa wamejitokeza kusaidia mashindano haya. Wametupa faraja na moyo wa kuendeleza mchezo huo, bado tunaomba wadhamini wajitokeze kudhamini mashindano haya. Ni mashindano ya kupima vipaji vya waogeaji wetu ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano haya,” alisema Shebe.

Mwandishi kabla ya kuposti asahihishe kasoro za maneno.
ReplyDelete