Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
SIKU chache baada ya kusikika kuwa Kocha raia wa Burundi, Thierry Hitimana kutangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Kocha huyo rasmi ametangazwa na Klabu ya Simba kama Kocha Msaidizi kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni baada ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Didier Gomes Da Rosa kutajwa kukosa vigezo vya Leseni inayotakiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kukiongoza Kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi msimu huu wa mashindano ya CAF, Gomes akitajwa kwenye orodha hiyo sambamba na Makocha wengine nane kutoka timu mbalimbali za Klabu barani Afrika.
Katika kuliweka sawa suala hilo, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Oscar Milambo amesema kuwa CAF wanataka sifa ya Leseni CAF A Diploma lakini kwa Makocha wa kigeni inahitajika zaidi ya sifa hizo ili kuongoza timu zao kwenye mashindano yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
“Kila Bara duniani lina taratibu zake, sisi bara la Afrika wanataka Mkufunzi awe na leseni ya CAF A Diploma kwa bara lote, lakini kwa Wakufunzi kutoka nje ya bara letu anatakiwa kuwa zaidi ya sifa hizo awe na UEFA A PRO ambayo ni sawa na CAF A Diploma”, ameeleza Milambo.
Milambo ameeleza kuwa hatua hiyo ya CAF ni kutaka kuboresha na kuwa na maendeleo zaidi kwa Wakufunzi wa Soka kuwa na sifa za juu katika kufundisha Soka barani Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...