Na Mwamvua Mwinyi,KIBAHA
MKUU
wa wilaya ya Kibaha ,mkoani Pwani ,Sara Msafiri ameeleza kuandika wosia
siyo uchuro kwani unasaidia kuondoa migogoro na kuepusha watoto kukosa
haki zao za msingi mara baada ya kiongozi wa familia kufariki dunia.
Aidha amesema baadhi ya akinamama wamekosa haki zao kwa kutokujua taratibu za kisheria mara inapotokea migogoro ya ndoa.
Msafiri
aliyasema hayo mjini Kibaha wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa
vijiji, mitaa na kata juu ya mauala yakiwemo usajili wa ndoa, talaka,
usimamizi wa mirathi, uandishi na utunzaji wa wosia na muunganisho wa
wadhamini na taratibu zake yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi
na Udhamini (RITA).
Alisema
kuwa baadhi ya ndoa zimekuwa na changamoto na kusababisha baadhi ya
wanandoa kuuana hivyo wanapaswa kumtanguliza Mungu na kufuata taratibu
za kisheria ili watambulike kisheria kuliko kuishi kienyeji.
Hata
hivyo ,alibainisha kuwa moja ya changamoto ya ndoa ambayo aliishuhudia
ni mume ni kuua mke wake kisha kumchoma kwa mkaa ambapo aliweka magunia
manne ya mkaa kisa walikuwa na ugomvi kwa miaka mine ambapo kila mtu
alikuwa anakaa chumba chake.
“Kisa
cha kumuua eti alikuwa akifikiria ametumia fedha nyingi kupata mali
halafu mke akidai talaka inabidi wagawane ndiyo sababu kuu ya kumuua na
kujifanya mke wake kapotea hivyo kuna haja ya viongozi kutoa elimu kwa
jamii kuhusu masuala mazima ya ndoa ”alisema Msafiri.
Akizungumzia
juu ya wosia alisema kuwa siyo uchuro bali ni kuweka mazingira mazuri
hata kiongozi wa familia akifa warithi wake kila mtu atajua haki yake
iko wapi na nini atarithi kutokana na jasho lake na wasitoe wosia wakiwa
kwenye hali mbaya au wengine wakiwa hoi hospitalini ambapo pia baadhi
ya wasimamizi wa mirathi wengine wanawatapeli warithi halali.
“Tumeshuhudia
baadhi ya watu ndani yafamilia wakiibuka bada ya kiongozi wa familia
kufa akidai za marehemu naye anasehemu ya kurithi na kuwaacha watoto au
mke ambao ndiyo warithi halali wakihangaika kama vile marehemu hakuacha
chochote,”alisema Msafiri.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria wa (RITA)
Lina Msanga alisema kuwa baaadhi ya watu wamekuwa wakihofia kutoa wosia
wakidai kuwa ni uchuro ambapo ni mwarobaini wa wale wanaoudhulumu mali
za marehemu ambapo kuna wosia 810 umehifadhiwa kwao.
Msanga
alisema kuwa ili kuhakikisha familia zinaishi kwenye hali nzuri wanatoa
elimu kwa viongozi mbalimbali hapa nchini ili wasaidie kuelimisha jamii
juu ya masuala ya familia na haki za jamii ambapo kuna mashauri 104 kwa
ajili ya kuyapatia ufumbuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...