Na Jamaly Mussa, DSJ

MWANADADA mwenye sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni katika muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo fleva Maua Sama ametangaza rasmi kupona matatizo yake ya kutokusikia vizuri pamoja na kinywa yaliyokuwa yakisumbuliwa kwa muda wa miezi saba.

Amesema kwa sasa amepona na yupo tayari kuendelea na kazi ya muziki kutokana na kukaa kimya muda mrefu huku akiweka wazi namna ambavyo amejiweka sawa kimuziki kuhakikisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanapata burudani ya nguvu.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Maua Sama kwa zaidi ya miezi saba alikuwa akisumbuliwa na matatizo hayo na kumfanya awe kimya kwa kutoachia kibao chochote ndani ya muda wote huo." Kwa sasa najiandaa na mtanisikia tena."

Katika ukimya wake huo uliosababishwa na matatizo yake ya kutosikia vizuri na kinywa, amethibitisha kupona kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema hivi; "Hey lovers Mungu wetu ni mwema...tatizo langu la kupoteza uwezo kusikia(Tinnitus) kwa zaidi ya mieza na matatizo ya kinywa sasa nimepona! Mungu ni mwema" amesema Maua Sama.

Kutokana na taarifa hiyo njema, sasa ni wakati wa Maua Sama kuachia ngoma kali kama ilivyo kawaida yake na kabla ya kukaa kimya kibao chake cha mwisho kilikua ni "Chuchumaa" na alimshirikisha msani wa Nyoshi El Sadaat na alitoa wimbo peke yake bila ya video.

Staili yake ya uimbaji wa kipekee ndio inayompa umaarufu mkubwa.Mashabiki wanakumbuka wimbo wake wa Iokote,ulibamba hatari na baadae  akaibuka na wimbo wa Can Dance.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...