Na Jamaly Mussa, DSJ.
STAA na mwanamitindo kutoka nchini Marekani Kylie Jenner amethibitisha kuwa na ujauzito wa msanii Travis Scott.
Kupitia ukurasa wake wa Instagramu mwanamitindo huyo anayejihusisha na uuzaji wa bidhaa zake za urembo kama Kylie Cosmetics ameweka video fupi ikionesha ameshika kipimo cha mimba akimuonesha mpenzi wake Scott baada ya kupata majibu ya vipimo vya mimba kikionyesha ana ujauzito.
Mwaka jana wa 2020 zilisambaa tetesi za wapenzi hao kuachana baada Kylie Jenner kuonekana kwenye gari la mpenzi wake wa zamani msanii Tyga. Hivyo kutokana na ujauzito huo inaonesha kuwa wapo pamoja katika penzi zito.
Wawili hao wamekuwa katika mahusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2017 na walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Stormi Februari mwaka 2018.
Aidha ujauzito huo ni wa pili wakiwa pamoja na msanii huyo tokea walipopata mtoto wao wa kwanza Februari mwaka 2018. Wapenzi hao wamekuwa wakisapotiana katika shughuli wanazozifanya huku mmoja akijishughulisha na urembo mwengine akijishughulisha na muziki na utayarishaji muziki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...