NA TIGANYA VINCENT
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limetoa miezi minne kwa kwa Watendaji wanaohusika na ukusanyaji mapato kuhakikisha wamefisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ifikapo Desemba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolelewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.
Alisema miezi ya kukusanya mapato kupitia vyanzo vya ndani imebaki mine ni vema watendaji wakahakikisha wanashirikiana na Madiwani ili watumie miezi iliyobaki kufikia malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi bilioni 2.4.
Ntahondi alisema Desemba shughuli za kilimo zikianza kama watakuwa hawajaifikia lengo itakuwa vigumu kukusanya kiasi walichojipangia.
Aliwataka Madiwani kuhakikisha wanawasimamia kwa karibu Watendaji wa vijiji ili waweze kuonyesha mpango wao wa ukusanyaji wa mapato na wautekeleze kwa vitendo.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori alisema wakusanyaji wa mapato wanatakiwa kuwa waadirifu kwa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa zinakwenda sehemu husika.
“Ndugu zangu Madiwani hakikishe kila senti ya Serikali inayokusanywa inapelekwa katika shughuli za maendeleo ya wananchi…pia hakikishe mnaziba mapengo ya upotevu wa mapato ya Serikali”alisitiza.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiimba wimbo wa Taifa kabla Baraza lao halijaanza jana
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...