Waogeleaji waliofikia viwango vya kamatin ya ufundi ya Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA) ndiyo wanaoruhusiwa kushiriki katika mashindano ya wazi ya klabu bingwa ya Taifa yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana Septemba 25 na 26.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe katika maohijiano na gazeti hili.
Hadija alisema kuwa wameamua kuweka sheria hiyo kwa lengo la kupata washindani wa kweli ilikuwapanafasi makocha wa timu ya taifa kufanya tathmini ya waogeleaji kwa ajili ya uteuzi wa timu za taifa kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Alisema kuwa hatua hiyo pia italeta ushindani kwa waogeleaji katika klabu zao na kuchagua waogeleaji waliokidhi masharti hayo.
Hadija alisema kuwa wanatarajia kuwa na waogelaji zaidi ya 150 kutoka klabu mbalimbali hapa nchini.
Shebe alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji wenye umri kuanzia miaka tisa (9) na wenye miaka 15 na zaidi katika mashindano hayo yaliyodhaniwa na Samsa Logistics Limited, Sapphire Court Hotel limited, Selcom Paytechltd, Pepsi, Azam, Gymkhana Club, Tarmal Industries ltd, Tanpack na Flames Restaurant.
Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la miaka tisa na 10, 11 mpaka 12, 13-14, na 15 ambapo muogeleaji atakayeibuka wa kwanza atapata pointi 20 ambapo wa pili na tatu watapata pointi 16 na 14 kila mmoja.
“Waogeleaji watakaomaliza katika nafasi ya nne watapata pointi 12 ambapo wa tano, sita, saba, nane, tisa na 10 watazwadiwa pointi 10, 8, 6, 4, 2 na moja. Haya ni mashindano ya TSA na yapo kwenye kalenda ya chama, hivyo waogeleaji wenye vigezo wanatakiwa kushiriki katika mashindano haya,” alisema.
Alisema kuwa jumla ya staili tano za kuogelea zitashindaniwa katika mashindano hayo ambazo ni backstrokes, butterflies, individual medleys, breaststrokes na freestyles.
“Tunawashukuru wadhamini ambao mpaka sasa wamejitokeza kusaidia mashindano haya. Wametupa faraja na moyo wa kuendeleza mchezo huo, bado tunaomba wadhamini wajitokeze kudhamini mashindano haya. Ni mashindano ya kupima vipaji vya waogeaji wetu ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano haya,” alisema Shebe.
Waogeleaji wa klabu mbalimbali wakijifua kuelekeaa mashindano ya wazi ya taifa ya kuogele yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana Septemba 25 na 26
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...