MJUMBE wa baraza la vijana Wilaya ya Mkuranga, Mariam Ulega amekutana na baraza la vijana wa Kata ya Mkamba kwa ajili kusikiliza kero pamoja na kufanya utatuzi.
Akizungumza vijana hao Bi Mariam aliwataka vijana kukijenga chama pamoja na vijana kuwa wamoja ili kufika malengo yao katika fursa zinazowazunguka kutokana na serikali kujenga miundombinu ya kuwafanya kuinuka kiuchumi.
Mariam Ulega aliweza kuwachangia vijana juu ya kuanzisha mradi wa UVCCM na kuahidi kuichangia matengenezo ya Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Kata ya Mkamba
Aidha aliahidi Bi Mariam aliahidi kuchangia kiasi cha shilingi laki tatu na kuwapa mipila saba (7) nakuwaahidi kuchangia sh.milioni mbili kwa Kata ya Mkamba kwa ajili kuendeleza baraza la vijana wa kata hiyo.
Diwani kata ya Mkamba,Hassan Dunda amempongeza Mjumbe wa Vijana kwa kuwaunga mkono vijana wa kata hiyo na kuwaongezea nguvu.
Mmoja wa Vijana wa Kata hiyo Said Juma amempongeza mjumbe kwa kuwaona vijana wa kata hiyo pamoja na kutatua baadhi ya kero zinazowakabili vijana .
Mjumbe wa Baraza la Vijana Wilaya ya Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na Vijana wa Kata ya Mkamba katika Baraza la kata hiyo wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Mkuranga, Mariam Ulega akikabidhi mipira saba (7) kwaajili ya kufanyia mazowezi vijana wa kata hiyo.
Mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akifunguwa Kijiwe cha UVCCM kata ya Mkamba Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Michuzi TV)
Mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Wilaya ya Mkuaranga Mkoa wa Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...