“Nimekuja kuchukua gari yangu, nimeacha mke na watoto nyumbani nimewambia nakuja kuchukua gari yangu, niliweka nia nimekuja kwa basi lakini sitarudi tena kwa basi,” anasema Dickson Joel mkazi wa Shinyanga ambaye amejinyakulia gari mpya aina ya Toyota RAV4 yenye thamani ya Sh milioni 136
Dickson Joel mkazi wa Shinyanga, ameshinda gari hiyo mpya baada ya kuibuka kidedea katika fainali za betPawa jana jioni.
Joel alikuwa miongoni mwa washindi wanane wa bahati nasibu hiyo ya kubashiri matokeo aliyeingia kwenye fainali, washiriki wengine walitoka kwenye mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa, Mtwara na Dar es Salaam.
"Wote wanane waliingia kwenye fainali baada ya kubashiri na BetPawa na kuingia kwenye droo ya kushindania gari mpya," alisema meneja masoko wa BetPawa, Job Ngaula.
Alisema katika fainali, washiriki wote wanane walitakiwa kupiga penalti tatu kila mmoja na waliopata zote ndiyo waliingia fainali ya mwisho ya kuwania gari hiyo.
Joel na Saddam Sudi waliingia kwenye fainali, na kutakiwa kupiga penalti tano kila mmoja ambapo Jeol alishinda kwa mikwaji ya penalty 5-3
Akizungumzia ushindi huo, Joel alisema ni kutokana na kutokata tamaa, kwani mara kadhaa amekuwa akibashiri matokeo bila kushinda.
"Hata hii ya sasa, nilibashiri lakini sikushinda mechi zile, lakini nilijaza kwa ufasaha mkeka wangu nikabahatika kuingia kwenye droo kubwa zaidi ya kuwania gari ambalo leo 'jana' nitaondoka nalo kwenda Shinyanga,".
Alisema yeye ni mzoefu na kupiga penalti na amekuwa akifanya mazoezi mara kwa mara na amekua akicheza mechi mbali mbali za mtaani hivyo hakupata shida kwenye fainali.
Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Mr Mr Eazi, alisema hiyo ni sehemu ya uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi ya EPL ambayo mechi zake ziko katika mchezo wa betting za BetPawa ambayo ni miongoni mwa kampuni za tasnia ya michezo ya kubashiri matokeo.
“Ni furaha kuwepo Tanzania na kuona mshindi akinyakua ndinga, Betpawa inajali watu wa chini na kuwapandisha juu, hivyo hivyo hata mimi muziki wangu naimbia watu wa chini ambao wamenipandisha na kunifikisha juum,” alisema
Kwa upande wa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo Mfuru na mwakilishi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Haule Philipo waliwapongeza washiriki wote kwa hatua waliyofikia, ambayo mbali na bingwa kuondoka na gari, washindi wa pili hadi wa sita walipewa zawadi ya PS5 na wa saba na wanane walipewa vocha ya kufanya manununzi ya Tsh 500,000.
Dickson Joel mkazi wa Shinyanga ambaye amejinyakulia gari mpya aina ya Toyota RAV4 yenye thamani ya Sh milioni 136 baada ya kuibuka kidedea katika fainali za betPawa jana jioni,pichani kulia akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr Mr Eazi
gari mpya aina ya Toyota RAV4 yenye thamani ya Sh milioni 136 aliyokabidhiwa Dickson Joel mkazi wa ShinyangaBaadhi ya washiriki wote wanane walitakiwa kupiga penalti tatu kila mmoja na waliopata zote ndiyo waliingia fainali ya mwisho ya kuwania gari hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...