Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la uhamiaji na mkuu wa uhamiaji mkoa wa Njombe, John Yindi akizungumza na vyombo vya habari namna wanavyopambana ili kuendelea kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini bila ya kibali

Na Amiri Kilagalila,Njombe
RAIA mmoja kutoka nchini Burundi ambaye alikuwa akitafuta vibarua ili apate fedha ya kujikimu,amehukumiwa kwenda jela miezi sita mkoani Njombe kwa kushindwa kulipa faini kiasi cha shilingi laki tano baada ya kukamatwa mkoani humo akiishi nchini bila kuwa na kibali.


Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la uhamiaji na mkuu wa uhamiaji mkoa wa Njombe, John Yindi amesema hayo mkoani humo wakati alipokuwa akielezea hatua mbalimbali ambazo jeshi la uhamiaji mkoani Njombe limekuwa likizichukua kudhibiti wahamiaji haramu wasiofuata taratibu za kuingia nchini wanasakwa.

“Katika mwezi huu tumefanikiwa kumkamata raia mmoja wa Burundi ambaye tayari amehukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini laki tano lakini ameshindwa kulipa sasa hivi ameenda gerezani.Huyu raia inasemekana ametokea mkoa wa Ruvuma lakini alikuwa anatafuta vibarua maeneo mbali mbali”alisema John Yindi

Mbali na raia huyo kufungwa jela, Mkuu huyo wa Uhamiaji mkoani Njombe amezungumzia namna wanavyoendelea kufanya doria kwenye barabara kuu ya kutoka Iringa kwenda Tunduma pamoja na utoaji wa elimu shirikishi kupitia Uhamiaji Kata ili kuwafichua wahamiaji haramu.

“Kwa sasa tunaendelea na doria ya kila siku katika bara bara kuu iendayo nchi ya jirani ya Zambia na Malawi lakini pia DRC,lengo ni kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu wa sheria za uhamiaji wanakamatwa pia tunaendelea na zoezi la utoaji wa elimu katika kata zote ili kuwapa elimu ya kuwatambua wageni mbali mbali”alisema Yindi
Aidha ametoa wito kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mpaka wa Tanzania na nchi ya Malawi katika mwambao wa ziwa Nyasa kuhusu kutoa ushirikiano kwa jeshi la uhamiaji.

“Nitoe wito kwa wavuvi kule kwamba kila anapopata mtu ambaye hajulikani kama mtanzania watoe taarifa haraka kwa mtendaji wa kata,kijiji au ofisi ya uhamiaji”aliongeza Kamanda Yindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...