Na John Walter-Manyara.

JESHI la Polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia mwanamke Janeth Doto Vicent ambaye ni mkazi wa  Mji wa Babati kwa tuhuma za kumchoma  mtoto wake wa kike sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Marrison Mwakyoma amethibitisha leo Septemba 14,2021 ambapo amesema tukio hilo Septemba 12 mwaka huu saa tatu asubuhi katika mtaa wa Mrara Juu.

"Mtoto huyo wa miaka mitatu alichomwa  sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali baada ya kuchukizwa na kitendo cha mtoto wake kuomba fedha kwa mpita njia,"amesema.

Kamanda Mwakyoma amesema kitendo hicho kilimfanya mama huyo kumchoma usoni na shingoni na kumsababishi majeraha ndipo wasamaria wema walivyoona kitendo hicho waliamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo,kwa sasa mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati, Mrara akiendelea na matibabu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...