Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MAMLAKA
ya Udhibiti Ununuzi wa Umma PPRA imetoa mafunzo kwa wakuu wa vitengo
vya manunuzi na ugavi 900 wa Halmashauri hapa nchini ili kupata uelewa
zaidi juu ya masuala hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo ,wakati wa mafunzo juu ya
taratibu sheria na kanuni za manunuzi ya umma ,Frank Yesaya ofisa
manunuzi na ugavi ,alisema mafunzo hayo yalitolewa kwa kipindi cha mwaka
mmoja uliopita.
Pia
aliwataka maofisa hao kufuata Sheria za manunuzi ili kuepukana na
hoja ambazo zinaweza kujitokeza wakati ukaguzi wa mikataba ya miradi
mbalimbali ambayo inatekelezwa katika halmashaurli hizo.
Awali
akifungua mafunzo hayo katibu tawala wa mkoa wa Pwani , Mwanasha Tumbo
aliwataka maofisa hao kusimamia manunuzi na mikataba mbalimbali ya
miradi ya maendeleo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi.
Ismail
Kiwela mwenyekiti wa halmashauri Chalinze,alishukuru kupata uelewa juu
ya masuala ya manunuzi na namna halmashauri inavyotoa tenda na kutafuta
mawakala ili kutekeleza masuala ya maendeleo.
Alisema, ni jukumu lao kuwa mabalozi wa kwenda kusimamia manunuzi na mikataba inayotolewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...