Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MTAA wa Muheza,Kata ya Mailmoja ,Kibaha ,mkoani Pwani ,inatarajia kuhesabu watu na makazi katika zoezi la sensa ya majaribio ,itakayofanyika siku tatu kuanzia tarehe 10 usiku wa kuamkia tarehe 11 September hadi 13 ,Mwaka huu.

Akielezea kuhusiana na utekelezaji ya sensa ya majaribio ,wakati wa kikao Cha kamati ya sensa  ,mratibu wa sensa wilaya ,Wambura Yamo alieleza ,kwa mwaka 2021 serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendesha sensa hiyo ya majaribio katika mikoa kumi na moja Tanzania Bara, na miwili Zanzibar.

Alisema ,imeanzwa kutekelezwa katika maeneo husika kuanzia septemba 8 hadi September 19 mwaka huu.

"Mkoa wa Pwani ikiwa ni iyoteuliwa miongoni mwa mikoa 11 Tanzania Bara iliyoteuliwa kufanyia sensa ya majaribio katika kata ya Muheza "alifafanua Wambura.

Aidha alibainisha ,kuanzia septemba 8 hadi 10 ni siku tatu ambazo makarani watatambua ramani ya eneo la kuhesabia a huduma za jamii ikiwemo shule,vyanzo vya maji,vituo vya afya,zahanati ,maduka ya dawa,kaya za jumuiya kama magereza ,vituo vya kulelea wazee na watoto ,kambi za wavuvi na wasio na makazi maalum ,wasafiri.

Wambura aliweka bayana ,tarehe 14 September hadi 16 September mwaka huu itahusu makarani kuhesabu nyumba na majengo.

"Tarehe 17 September hadi 19 September mwaka huu itahusu makarani kuhesabu anuani ya makazi"

Wambura alisema ,sensa hiyo inafanyika ili kufanikisha ubora na ufanisi wa vitendea kazi yenye teknolojia mpya itakayotumika kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 agost 28.

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha , Sara Msafiri alieleza, serikali inatumia fedha nyingi kutekelezwa zoezi hili muhimu hivyo wananchi hao wasiiangushe wilaya .

Msafiri alisema,anaamini watafanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na kuongeza'" ametaka walengwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili majaribio yaleta matokeo chanya.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...