Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania Omari M. Dibibi amefunga rasmi kikao  cha majadiliano ya maslahi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta na kufikiwa maamuzi ya kuwasilishwa katika Baraza la majadiliano la Shirika hilo.

Kikao hicho kilichofunguliwa nana na Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo kimeweza kuangalia maslahi mapana ya mfanyakazi wa Shirika hilo katika sera ya Ukimwi na mazishi kwa wafanyakazi.

Baada ya majadiliano ya siku mbili, Kikao hicho kimefungwa rasmi na kilihudhuriwa na  na viongozi wa vyama vya wafanyakazj, menejimenti na wawakilishi wa menejimenti ya Shirika la Posta nchini, katika ukumbi wa Edema, Mkoani Mororgoro.

Baraza hilo limeweza kupokea sera mbili zilizowasilishwa na menejimenti ya Shirika la posta zinazohusiana na masuala ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi  pamoja na masuala yanayohusu mazishi kwa wafanyakazi wa shirika hilo lengo likiwa ni kuweka mazingira rafiki kwa watendaji wa Shirika wake.

Aidha, sera hizo zinaenda kuleta usawa kwa wafanyakazi wa Posta bila kuzingatia dini wala vyeo katika masuala yote ya misiba pindi inapotokea mfanyakazi amefariki au amefiwa na mtoto au mzazi.

Vilevile kupitia Baraza hilo, Menejimenti ya Shirika la Posta imewasilisha pia sera ya UKIMWI ambayo inaitaka Shirika kuwapa elimu wafanyakazi namna ya kujikinga na kujilinda na maambukizi hayo.

Sambamba na hilo, sera hiyo imelitaka Shirika kuweka mazingira wezeshi kwa watendaji wake wanaoishi na magonjwa hayo.

Kikao hicho kimekaa kwa muda wa siku mbili kililienga kujadili maslahi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta nchini na kilifunguliwa na Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Daniel  Mbodo September 8, 2021.

Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania, Omari M. Dibibi akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Majadiliano cha Baraza hilo kilichojadili maslahi ya wafanyakazi  na kwa pamoja kuamua kupeleka kwenye Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania (TPC)
Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Aron Samwel akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la majadiliano, kilichokuwa kinaendelea, mkoani Morogoro.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania Mabrouk Makame akifurahia jambo na wajumbe wa Baraza hilo, mara baada ya kufungwa kwa kikao cha Baraza la Majadiliano kilichomalizika kwa maamuzi ya pamoja ya kupeleka sera mbali katika baraza la majadiliano la TPC





 Wajumbe wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania wakijadili hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Baraza hilo kilicholenga kujadili maslahi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta, kabla ya kufungwa kwa kikao hiko, katika ukumbi wa Edema, Morogor

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...